Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda Jumamosi Februari 1, 2025 amewaongoza Mamia ya Wana Mazoezi Katika Mazoezi ya Viungo yaliyofanyika Katika mji wa Shelui yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Shelui.
Akizungumza baada ya Kushiriki Mazoezi hayo DC Mwenda amewasisitiza Wananchi kuendelea kufanya Mazoezi ili kuimarisha afya zao na kuepuka Magonjwa yasiyoambukiza.
Aidha Mwenda ameeleza kuwa Maradhi yasioambukiza ikiwemo Kisukari,Presha, Unene uliopitiliza Shinikizo la Moyo yamekuwa Tishio la Kiafya hivi sasa lakini yanaepukika kwa jamii kufanya mazoezi.
"Wapo wenzetu wengi wamejipatia ajira kupitia Michezo na wanalipwa Fedha nyingi kupitia vipaji vyao,Tujiwekee ratiba kwa Wananchi wetu kufanya mazoezi na Wanafunzi wetu tuhakikishe ratiba ya Michezo inatekelezwa kikamilifu ."Amesema DC Mwenda.
DC Mwenda amewahakikishia wanamichezo Wilayani Iramba kuwa azma yake ya kugawa vifaa vya Michezo Iko palepale na wake wote watakaofanya vizuri nitatoa seti ya vifaa vya Michezo kusisitiza kuwashawishi Watu wengi zaidi kufanya Mazoezi
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Shelui Agnes Nassania amemuhakikishia DC Mwenda kuwa wanejipanga kuhakikisha wanaendeleza mazoezi hayo kwa lengo la kuimarisha Afya dhidi ya magonjwa yasiyoambukizwa.
"Nikuhakikishie Kiongozi wetu,Shelui tutaendelea kufanya mazoezi kwa lengo la kuimarisha Afya zetu na kuibua vipaji vya Vijana wetu kuanzia ngazi ya Vitongoji na Vijiji". amesisitiza Diwani Kata ya Shelui Agnes Nassania.
Wilaya ya Iramba imejiwekea utaratibu wa kuhakikisha Wananchi wote wanashiriki kwenye mazoezi ili kuimarisha Afya zao,Mazoezi haya ni endelevu na zawadi mbalimbali zitatolewa kwa wale wote watakaoshiriki kwenye mazoezi kwa ajili ya kuimarisha Afya.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.