Timu ya Uendeshaji huduma za Afya Wilaya (CHMTs) na Wakuu wa vituo vya kutolea huduma za Afya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida wametakiwa kutoa elimu ya umuhimu wa chanjo kwa jamii ili kurahisisha shughuli hiyo ya utoaji chanjo itakavyoanza badaye mwezi huu.
Kauli hiyo imetolewa Ijumaa Disemba 6,2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Ndugu Michael Agustino Matomora katika kikao cha tathmini ya takwimu za idara ya afya kwa robo ya mwezi julai hadi septemba 2024 na maandalizi ya wiki ya chanjo.
Amesema pamoja na kutoa elimu kwa wananchi wahakikishe wanawatafuta watoto waliohasi chanjo ili wapate huduma hiyo itakayowasaidia kujilinda na maradhi mbalimbali.
“Kwa sasa tuna asilimia 5 ya watoto waliohasi chanjo, tukawatafute na kuwapa chanjo pamoja na kuweka mikakati endelevu ya kuzuia kuhasi tena chanjo hizi.” Alisema Matomora.
Aidha, Matomora alielekeza kuboresha viashiria vya afya ya uzazi na mtoto ikiwa ni pamoja na kuweka mkakati wa kuhakikisha wajawazito wanajifungua katika vituo vya afya, mbapo kwa sasa ni asilimia 83 ya wajawazito wanaojifungua katika vituo hivyo ikiwa ni chini ya lengo la asilimia 95.
Pia amesisitiza kuhusu utekelezaji wa sera ya uzazi wa mpango ili kufikia malengo ya Serikali katika sera hiyo.
Akitoa takwimu za chanjo kwa robo ya Julai hadi Septemba Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Dkt. Glory Cleophace Andrew alisema bado kuna changamoto ya baadhi ya watoto ambao hawapati chanjo na hivyo kwa sasa imewekwa mikakati ya kuzuia hali hiyo ili kuondoa hatari ya magonjwa ya milipuko.
“Kwa mwaka uliopita kulikuwa na milipuko ya surua, baadhi ya maeneo lakini pia Wilaya ya Iramba ilitugusa kidogo. Pia Kuna magonjwa mengine ambayo kama hatutafanya shughuli hii ya chanjo vizuri milipuko hii inaweza ikatokea” Alisema Dkt. Gloria Cleophace Andrew
Wiki ya chanjo inatarajiwa kuanza Decemba 16, 2024 na itakamilika decemba 20 mwaka huu kwenye vituo vyote 49 vinavyotoa huduma ya chanjo.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.