Naibu waziri wa afya, jinsia wazee na watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile (Mb) amefanya Ziara ya Kikazi wilaya ya iramba. Katika ziara hiyo Mhe; Dkt Ndungulile amezindua mradi wa maji katika kijiji cha Ruruma Wilayani Iramba Mradi huu wa maji katika kijiji cha Ruruma ni mmoja wapo ya shughuli ambazo mradi wa world vision umekuwa ukitekeleza kwa kushirikiana na jamii/Wadau mbalimbali na umetekelezwa kwa ufadhili wa world vision UK(Uingereza). Aidha mradi huu ulitokana na hitaji la jamii husika katika kukabiliana na changamoto ya Upatikanaji wa maji safi na salama.
Mradi huu ulitekelezwa katika awamu mbili: awamu ya kwanza ilikuwa ni utafiti na uchimbaji wa kisima kirefu ambao ulifanyika kwa mwaka wa fedha 2016/2017
Awamu ya pili ilikuwa ni usambazaji wa maji pamoja na ujenzi/ununuzi wa tanki la kuifadhia na kusambazia maji vituo vikuu vinne vikiwemo vituo katika shule ya msingi Ruruma pamoja na zahanati ya kijiji cha Ruruma ambayo ilitekelezwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Mradi huu unategemea kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo lililokuwepo la Upatikanaji wa maji safi na salama kwa kuwanufaisha kaya 813 wakiwemo watoto na akina mama ambao ndiyo waliokuwa wakipata shida Zaidi kwa kuchimba madimbwi mitoni kwa nia ya kupata maji ambayo pia hayakuwa salama kwa afya/Matumizi ya binadamu.
Aidha taasisi zinazofaidika pia na huduma/mradi huu ni pamoja na zahanati ya kijiji yenye uwezo wa kuhudumia watu 45 kwa siku pamoja na shule ya msingi yenye Jumla ya wanafunzi 584 na walimu 10.
Mradi huu mpaka kukamilisha umegharimu fedha za Kitanzania Tsh. 154,617,776/=. Mradi huu ulikamilisha na kukabidhi kwa jamii vyoo vilivyo gharimu Tshs. 21,000000 kwa ajili ya wanafunzi wa kike na kiume vyenye Jumla ya matundu 8 ikiwa ni pamoja na chumba maalum cha kujisitiri kwa ajili ya wanafunzi wa kike.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.