▪️Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawasalimia Wana Singida na anawapongeza kwa kazi kubwa ya ujenzi wa Taifa.
▪️Mradi wa SGR ni wa kimkakati una manufaa kwa Taifa letu, ni uti wa mgongo wa Taifa letu, hapa Singida tutanufaika na mradi huu.
▪️Katika Siku 100 Rais Dkt. Samia ameweka vipaumbele ikiwemo kuanza kwa utaratibu matumizi ya Bima ya Afya kwa wote, anataka jambo hili lianze haraka.
▪️Sisi wasaidizi tutafuatilia kwa karibu ahadi zote za Rais Dkt. Samia, tutafuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi pamoja na kufuatilia miradi yote ya maendeleo ili kuwanufaisha Watanzania,
▪️Watumishi wa Umma wanaowasumbua Watanzania hawatakuwa na nafasi, haiwezekani mwananchi anaenda kwenye ofisi ya umma anatarajia apate ufumbuzi na huduma ila anafika pale anazungushwa, huu siyo uelekeo wa Rais Dkt. Samia anaotaka.
▪️Rais Dkt. Samia ametoa vitendea kazi anataka kuona Watanzania wanahudumiwa kwa ufanisi, Mwananchi akifika ofisini msikilize, weka kumbukumbu kisha fanyia kazi na likikuzidi lifikishe kunakostahili.
▪️Mkitaka wananchi wasibebe mabango wafikieni, wasilikizeni na muwatatulie kero zao, nimeitisha taarifa kila mkoa nikipita huko nikikuta kuna mambo yasiyofaa nitachukua hatua, hatuwezi kuwa nchi ya uchumi wa kati na watu hawatekelezi majukumu yao kikamilifu
▪️Tanzania ni mali ya Watanzania, si mali ya viongozi wala si mali ya vyama vya siasa, tuilinde nchi yetu, tusidanganywe kufanya vitendo visivyofaa, Mungu ametupa nchi nzuri sana.
▪️Tanzania hii imebarikiwa sana, tunayo madini adimi, gesi na rasilimali nyingine nyingi, tunajua haya ndiyo yanayowaumiza, Watanzania hatuna sababu ya kutofautiana, tukatae utaratibu ambao unaivunjia heshima nchi yetu, twendeni tukatatue kasoro hizi sisi wenyewe tuache nchi yetu ikiwa salama.
▪️Vijana na Watanzania wote tuipende na tuilinde nchi yetu, tuna mambo yanayohusu vijana, Rais Dkt. Samia ameanzisha Wizara ya Vijana ambayo itashughulikia masuala yote ya vijana.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.