Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda amewataka wagombea wote na vyama vya siasa vitakavyoshiriki kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kufanya kampeni za kistaarabu na zenye staha.
Mwenda ameyasema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye ziara yake ya kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo pamoja na Kusikiliza na Kutatua kero mbalimbali za Wananchi Novemba 7,2024 kwenye Vijiji vya Kata ya Kaselya
Aidha amesema kuwa Vyama Vyote vya Siasa vinavyoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Iramba,vinatakiwa kufuata Sheria na kanuni za uchaguzi za mwaka 2024.
"Ninatarajia vyama Vyote vitafanya kampeni za kistaarabu zinazozingatia Sheria na taratibu pia utu,Jengeni hoja wewe kiongozi unayeomba ridhaa kwa Wananchi waeleze wakikuchagua utawafanyia Nini Wananchi hao kwenye Kijiji chao au Kitongoji unachogombea" Amesisitiza Mwenda
Kiongozi huyo amewataka wagombea wote kutoka vyama vinavyoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuhakikisha wanaofanya kampeni za kistaarabu ili Wananchi waweze Kusikiliza sera na kufanya maamuzi sahihi.
"Wananchi wa Iramba wanataka huduma Bora kutoka kwa Viongozi wao, Wagombea jengeni hoja nzuri ukichaguliwa utawafanyia Nini Wananchi tunaowaongoza hatutaki kusikia usimchague fulani kwa sababu mkwewe alikamatwa ugoni,anakaa nyumba mbaya" Amefafanua DC Mwenda.
Mwenda amesema Serikali imejiandaa kikamilifu kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa ufanisi mkubwa katika Hali ya amani na utulivu ,Vyama mbalimbali vya Siasa vinashiriki kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.