Meneja wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Singida Bw. Almachius Mbekenga Raphael kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa GPSA Prof. Geraldine Arbogast Rasheli amekabidhi madawati 200 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba siku ya Jumanne tarehe 17 Desemba,2024 Mkoani Singida.
Madawati hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Msaada kwa Jamii katika Mpango Mkakati (2023/24-207/28) wa GPSA ambapo jumla ya madawati yatakayotolewa kwa mwaka huu ni 400.
Bw. Almachius Raphael alisema kuwa GPSA hutoa msaada kwa jamii katika sekta mbali mbali ikiwemo sekta ya Elimu ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya Elimu.
"Mwaka huu 2024/25 tumeamua kama Taasisi tutoe msaada katika sekta ya Elimu Wilaya ya Iramba ambapo tunatoa msaada wa madawati jumla 400. Kwa awamu ya kwanza tumeleta madawati 200 kwaajili ya matumizi ya shule," amesema Almachius Raphael.
Kwa upande wake Bw. Oswald Leopord (Afisa Tarafa, Tarafa Kisiriri) aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, ametoa pongezi kwa GPSA kwa kutoa msaada huo ili kuwawezesha wanafunzi kupata Elimu katika mazingira mazuri.
"Katika shule zetu bado tuna uhaba japo Serikali ya awamu ya sita imefanya jitihada kubwa kuhakikisha inaboresha sekta zote ikiwemo sekta ya Elimu, sekta ya Afya na miundombinu mingine. Hiki mnachokifanya GPSA nawapongeza sana."
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.