Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Mwenda ameishukuru Benki ya CRDB kwa kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Mukulu akisema kitasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha huduma za afya kwa wananchi wa Kata ya Mukulu na maeneo jirani.
Kutokana na uhitaji kuongezeka kila siku, Mheshimiwa Mwenda amesema serikali inafanya jitihada kubwa kuboresha huduma za afya na inawaikaribisha sekta binafsi kuongeza nguvu ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma katika maeneo jirani.
"Niwashukuru sana Benki ya CRDB kwa kutusaidia kukijenga, hakika ninyi ni benki ya mfano nchini,” amesema DC Mwenda.
Mwenda amesema hayo kwenye hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Kijiji cha Mukulu akimwakilisha Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba aliyeomba ujenzi wa kituo hicho cha afya kwa niaba ya wananchi.
Akikabidhi kituo hicho, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Dkt. Donald Mmari amesema ni utaratibu wa benki kutenga asilimia moja ya faida yake baada ya kodi kila mwaka ili kusaidia kutekeleza miradi inayowalenga wananchi.
“Mradi huu wa Kituo cha Afya Mukulu ni ushuhuda wa utekelezaji wa sera hiyo. Ujenzi wa kituo hiki unalenga kuboresha huduma za afya kwa wananchi na wakazi wa hapa. Ujenzi wake umefanyika kwa weledi na ushirikiano wa karibu baina yetu na halmashauri tukizingatia mahitaji halisi ya wananchi wa hapa Mukulu na Wilaya nzima ya Iramba,” amesema
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.