Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda amewataka Maafisa Watendaji Kata, Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu Wilayani Iramba, kila mmoja ahakikishe Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza wanaripoti na uandikishaji wa watoto wote wenye umri wa kuanza Elimu ya Awali na Darasa la Kwanza unafanyika na kukamilika mapema ili kuwapa fursa walimu kuendelea kufundisha.
Dc Mwenda amesema hayo Jumatano Januari 22, 2025 wakati akipokea Taarifa ya Kuripoti kwa Wanafunzi wa kidato cha Kwanza na Uandikishaji wa Wanafunzi wa Elimu ya Awali na darasa la kwanza wakati akizungumza na Wakuu wa idara na Taasisi za Serikali,Watendaji wa Kata,Maafisa Tarafa na Watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri
Amesema Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023 inasisitiza utoaji wa elimu bora, kuanzia Elimu ya Awali ambayo ndiyo msingi wa kwanza katika mfumo wa Elimu rasmi kote ulimwenguni. Pia amesema tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa Elimu ya Awali ina mchango mkubwa katika makuzi na malezi ya mtoto kiakili, kimwili na kijamii.
Aidha, amesema, Serikali imeendelea kutekeleza mpango wa elimu bila ada kuanzia Elimu ya Awali hadi Kidato cha Sita.
"Hakikisheni wanafunzi wa kidato cha Kwanza wanaripoti bila kudaiwa mchango Wowote kwa kuwa Rais wetu anatoa Fedha kupitia Elimu Bure na ifanyike oparesheni itakayowahusisha Watendaji wa Kata na Vijiji Maafisa Elimu Kata,Walimu Wakuu na kuwakamata Wazazi wote watakaoshindwa kuwapeleka Watoto shuleni" Alisisitiza DC Mwenda
Ameongezea kwa kutoa wito kwa wazazi wote wenye wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari wahimizwe kuwapeleka shule wanafunzi hao mepama iwezekanavyo ili kuepuka kukosa mafunzo kabilishi (orientation course) yanayotolewa kama msingi wa ujifunzaji katika ngazi hiyo ya elimu.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.