Halmashauri ya wilaya ya Iramba mkoani Singida imehitimisha mashindano ya michezo ya sekondari Tanzania (UMISSETA) kwa mwaka 2018 katika uwanja wa CCM Lulumba.
UMISSETA ni Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari hukutanisha wachezaji waliochujwa kutoka shule mbalimbali.
Mashindano hayo yamehusisha soka, Netboli, Kikapu, Bao, Kurusha Tufe, Mikono, Meza, wavu, na Riadhaa ambayo yameshirikisha shule za tarafa mbalimbali wilayani humo ambapo washindi wameshindanishwa na Tarafa ya Kisiriri kuibuka mshindi na hatimaye kupata timu ya wilaya.
Akizungumza na wachezaji kutoka shule za sekondari Tarafa Shelui, shule za sekondari Tarafa ya Ndago, shule za sekondari Tarafa ya Kinampanda na shule za sekondari Tarafa ya Kisiriri. Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe. Emmanule Luhahula aliwata wachezaji hao kuwa wamoja.
Mhe. Luhahula Alisema pamoja na kuwa wachezaji hao wanatoka shule mbali mbali wilayani humo wanapaswa kushirikiana na kupata ushindi pindi watakapo cheza na wilaya zingine kutafuta wawakilishi ngazi ya taifa.
Mkuu wa wilaya ya iramba aliongeza kuwa ninyi ni wamoja na mnatoka wilaya moja tunataka mtuoneshe ufundi wenu, vipaji na ushindani ili tupate timu bora zitakazoshindana na Mikoa mingine.
Ofisa Elimu Sekondari wa wilaya ya Iramba Bi. Elizaberth Lusingu aliwata wachezaji hao kucheza kwa juhudi na maarifa na kusema kuwa michezo ni upendo, huleta furaha pia kutoa ajira endapo wachezaji watajituma.
Machindano ya UMISSETA kimkoa yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 27 hadi 29/2018 katika Halmashauri ya wilaya Itigi mkoani Singida Wakati kitaifa yanatajiwa kufanyika Chuo cha Ualimu Butimba Mkoani Mwanza June 04 hadi 15 mwaka huu.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.