Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni ametoa pongezi na kupokea cheti cha ushindi wa Maonesho ya Nane Nane mwaka huu toka kwa wajasiriamali na wakulima walioshiriki maonesho hayo na kufanikiwa kupata ushindi ukilinganisha na Halmashauri sita na Manispaa moja za Mkoa wa Singida zilizoshiriki.
Pongezi hizo zimetolewa hivi karibuni wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi Mdogo wa Halmashauri hiyo mjini hapa.
“Nawapongeza sana kwa ushindi huu, hivyo Idara ya Kilimo iendelee kuwashawishi wakulima na wajasiriamali kujiandaa kwa maonesho yajao,” amepongeza Mwageni na kuongeza kuwa
“Kwa yule aliyebuni kifaa aina ya pawatila akiaswa kuongeza ubunifu ili awe na uwezo wa kuwa na mashine nzuri ya kusaga na kukoboa nafaka kwa ajili ya kusindika bidhaa na kuepuka kuuza mahindi gafi kwa sababu itakuwezesha kupata pumba na unga ambavyo vitakua na bei ya juu kibiashara,”
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo amemuahidi mbunifu huyo kumpatia mashine ya kuchomelea ili kuja kufanya kazi ya kutengeneza pawatila litakalokaa Halmashauri kama maonesho na kusaidia ubebaji wa taka ngumu katika maeneo mbalimbali ya mji wa kiomboi.
“Naomba ufahamu kuwa ukifanya kazi yenye viwango vizuri itakuwezesha kupata mtaji kupitia mikopo ya vijana inayotolewa na Halmashauri, kujiendeleza kiuchumi” amesema Mwageni
Wajasiriamali na Wakulima hao wameaswa kulitumia jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Iramba liliyopo katika viwanja vya Nzuguni Nane Nane kuwa ni fursa kwao kupeleka bidhaa mbalimbali ikiwemo mbogamboga, kambare, pelege na kamongo watokao ziwa Kitangiri na kutokusubiri wakati wa Nane Nane tu.
“Ni fursa kulitumia jengo hilo la kibiashara hasa kwa sababu lipo karibu na jengo la soko la Ndugai Jijini Dodoma, hivyo mtapata wateja tu,” ametilia mkazo Mwageni
Halikadhalika, amewataka wadau hao kwenda Nane Nane kwa ajili ya kutafuta na kutangaza soko la bidhaa wanazozalisha ili kujipatia wateja wakati wa Nane Nane na usio wa Nane Nane.
Mapema akitoa taarifa fupi mbele ya Mkurugenzi huyo Mwenyekiti wa Wajasiriamali na Wakulima hao, Flora Richard amesema kuwa wakulima na wafugaji wamefanikiwa kupata elimu ya juu ya teknolojia mbalimbali za kilimo, ufugaji na usindikaji.
Pia amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba imefanikiwa kupata ushindi wa nafasi ya kwanza kimkoa na kutoa mkulima bora kwa nafasi ya kwanza kikanda katika maonesho yaliofanyika Nzuguni Jijini Dodoma mwaka huu.
Naye Mshindi wa zao la mahindi kanda ya Kati, toka Wilaya hiyo kata ya Kyengege Kijiji cha Mgundu,
Yesaya Njolle amesema kuwa wamejifunza kuwa kilimo kinauwezo wa kumtoa Mkulima katika umasikini na kwenda kwenye hali ya kati ya maisha.
Ameongeza kuwa kilimo cha kisasa kwa wakati wa masika na kile cha kiangazi ikiwa masharti yatafuatwa kwa kuzingatia maarifa na weledi walioupata wanaouwezo wakupata mazao msimu wa kipwa na masika.
MWISHO
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni akipokea cheti cha ushindi wa maonesho ya Nane Nane mwaka huu toka kwa mweneyekiti wa Wakulima na Wajasiriamali walioshiriki maonesho hayo. Picha na Hemedi Munga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni akionesha cheti cha ushindi wa maonesho ya Nane Nane mwaka huu toka kwa mweneyekiti wa Wakulima na Wajasiriamali walioshiriki maonesho hayo. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.