HALMASHAURI ZAKUMBUSHWA KUTENGA BAJETI YA WANAMICHEZO SHIMISEMITA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amezitaka halmashauri zote kutenga bajeti na kugharamia ushiriki wa watumishi kwenye mashindano ya Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA).
Akizungumza kwa niaba yake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, alisema ni jukumu la halmashauri kuwawezesha watumishi kushiriki kwani michezo ni sehemu ya kazi.
Mashindano ya mwaka huu yameshirikisha halmashauri 152 kati ya 184, na wanamichezo 4,000. Aidha, Mhe. Burian aliipongeza Kamati ya Taifa kwa maandalizi bora na washindi wa michezo mbalimbali, akisisitiza mshikamano, afya na nidhamu kuwa malengo makuu ya mashindano haya.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.