Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amezindua majengo mapya na huduma ya upasuaji wa dharura kituo cha Afya Ndago kilicho jengwa kwa fedha zilizoletwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Luhahula amezindua huduma hiyo leo Jumatatu Machi 2, 2020 katika kiwanja cha kituo cha Afya Ndago Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu huyo wa Wilaya, amewataka wananchi kuyalinda majengo hayo vizuri kwa kuwa ni kumbukumbu kubwa katika mji wa Ndago.
“ Niwaombe wananchi wote kuyalinda majengo haya kwa sababu ni mali yetu ili yaweze kudumu,” amesama Luhahula na kuongeza
“ Niwaombe Wataalamu na Madaktari kuendelea kutoa huduma kwa weledi.”
Halikadhalika amewaomba Wananchi kujiunga na iCHF iliyoboreshwa ambayo inampa Mwanachi fursa ya kutibiwa hadi ngazi ya Mkoa kwa watu sita katika familia.
“Ndugu zangu hakikisheni mnajiunga na iCHF iliyoboreshwa na wala msisubiri muuguwe ndio mwende mkachajiwe fedha maana kama mtu hana iCHF iliyoboreshwa garama ni kubwa sana,” amesisitiza Luhahula
Awali akiwasilisha taarifa ya mradi mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mfamasia wa Wilaya Zuberi Abdallah amesema mradi umelenga kusogeza huduma za Afya hasa za dharura za uzazi kwa kinamama wajawazito, watoto na wananchi wote wa Tarafa ya Ndago.
Aidha ametumia fusra hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa Kuleta Tshs400 milioni zilizotumika katika ujenzi wa majengo hayo.
Pia amebainisha mchango wa mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo na fedha za wadau wa mfuko wa Afya wa pamoja (Performance Trenche) takribani Tshs61.52 milioni huku michango ya wananchi ikiwa ni Tshs8 milioni.
Ujenzi na ukarabati wa majengo hayo wenye jumla ya takribani Tshs469.528 milioni kujenga jengo la mama na mtoto, nyumba ya mtumishi, jengo la kufulia (laundry), jengo la kuhifazia maiti (mortuary), jengo la maabara (laboratory) na jengo la upasuaji (Theater).
Awali kituo cha Afya Ndago kilikuwa na uwezo wa kutoa huduma ya wagonjwa wanje (OPD), huduma ya kulaza wagonjwa (IPD), huduma za maabara, huduma ya Afya ya uzazi na mtoto, huduma ya tiba na malezi kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi (CTC).
Aidha kukamilika kwa majengo hayo kumewezesha fursa ya kuanza rasmi upasuaji wa dharura, hivyo kufanikiwa kuondoa adha ya wagonjwa wanaotoka maeneo ya ndago na vitongoji vyake.
Naye Mwenyekiti wa Huduma za Jamii, Kinota Hamisi amewataka wananchi kuto ihujumu miundombinu hiyo huku akiwahakikishia kuwa serikali italeta vifaa tiba na waganga hivi karibuni.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Ndago, Henry Nkandi amewataka wananchi hao kutumia fusra ya kuanzisha biashara kwa kuwa Ndago itapokea watu wengi watakaokuwa wakihitaji huduma mbalimbali.
“ Ndugu zangu tambueni kuwa Tarafa ya Ndago inakata 6, hivyo watu wote watakuja Ndago kupata huduma za Afya na nyinginezo hivyo fungueni biashara zitakazowahudumia hao,” amesema Nkandi
Naye mmoja wa Wazazi aliojifungua katika kituo hicho jana ambaye hakutaka jina lake lifahamike ameishukuru serikali na Madaktari wanaotoa huduma hapo kwa huduma nzuri wanazozipata na kupunguziwa garama walizokuwa wakizitoa kwenda Hospitali ya Wilaya Mjini Kiomboi.
MWISHO
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kushoto, Hussein Sepoko akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba wakienda kukagua majengo mapya na huduma ya upasuaji wa dharura kituo cha Afya Ndago katika siku ya uzinduzi wa majengo na huduma hiyo. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amezindua majengo mapya na huduma ya upasuaji wa dharura kituo cha Afya Ndago kilicho jengwa kwa fedha zilizoletwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Picha na Hemedi Munga
Mfamasia wa Wilaya ya Iramba, Zuberi Abdallah akisoma taarifa ya Mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Ndago uliogarimu takribani Tshs469.528 milioni. Picha na Hemedi Munga
Meneja wa Benki ya NMB mjini Kiomboi akiwaeleza wananchi waliohudhuria uzinduzi wa majengo mapya na huduma ya upasuaji wa dharura kituo cha Afya Ndago fursa zilizopo katika benki hiyo, ikiwa ni pamoja na akaunti ya mtoto,ukopeshaji wa ujenzi wa nyumba na mkopo wa ujasiriamali. Picha na Hemedi Munga
Wananchi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa majengo mapya na huduma ya upasuaji wa dharura kituo cha Afya Ndago . Picha na Hemedi Munga
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Simion Tyosela akiwashukuru wataalumu wa Afya na wote walioshiriki katika ujenzi wa majengo hayo tangu hatua ya awali mpaka kukamilika na kuzinduliwa. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula akimpokea mtoto aliozaliwa siku ya uzinduzi wa kituo cha Afya Ndago. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.