Timu ya riadha kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iramba inaendelea kuonyesha ubora wake katika Mashindano ya Michezo ya Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa Tanzania (SHIMISEMITA) yanayoendelea kufanyika jijini Tanga.
Tarehe 22 Agosti 2025, mwanariadha Verynice Meena alidhihirisha uwezo mkubwa baada ya kushika nafasi ya nne katika mbio za mita 200 (kundi B – wanawake), na hivyo kufuzu hatua ya nusu fainali ya mbio hizo.
Ufanisi huo unampa Meena tiketi ya moja kwa moja ya kushiriki hatua ya nusu fainali, jambo linaloongeza hamasa na matumaini kwa timu ya Iramba kuendelea kupeperusha vema bendera ya wilaya hiyo kwenye mashindano makubwa ya kitaifa.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.