Iramba Yaadhimisha Miaka 61 ya Muungano kwa Upandaji Miti pamoja na Mazoezi ya pamoja
Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, imeadhimisha miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kupanda miti katika Shule Mpya ya Msingi Yombo iliyopo kata ya Tulya, kufanya mkutano wa hadhara kuelezea historia na faida za Muungano, pamoja na kufanya matembezi ya kilomita tano kutoka kijiji cha Tulya hadi Doromoni.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika Aprili 26, 2025, yaliongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba, Bi. Bupe Mwakibete, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mhe. Suleiman Yusuph Mwenda. Akizungumza na wananchi, Bi. Mwakibete aliwasihi Watanzania kuendeleza na kuuenzi Muungano kwa kudumisha amani, mshikamano na upendo miongoni mwao.
"Tunaadhimisha miaka 61 ya Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar ambao ulituunganisha kuwa Nchi Moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ninawaomba Wananchi tuendelee kuutunza na kuuenzi Muungano wetu". alisema Bi. Mwakibete
Akiwakumbusha wananchi umuhimu wa Muungano, Bi. Mwakibete alisisitiza kuwa umekuwa msingi wa mshikamano wa kitaifa na maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni: "Muungano Wetu ni Dhamana, Heshima na Tunu ya Taifa: Shiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025."
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.