Mkuu wa Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, Suleiman Yusuph Mwenda, ameitaka jamii kushirikiana katika kuwalea Vijana/watoto kwa maadili mema kuanzia ngazi ya familia ili kuepusha mmomonyoko wa maadili.
Akizungumza katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika vijiji vya Kisimba, Kata ya Kisiriri na Kinambeu, Old Kiomboi, DC Mwenda alisema hakuna mzazi au mlezi anayefurahia kuona kijana/mtoto wake akijihusisha na tabia zinazokwenda kinyume na maadili ya Kitanzania.
“Jamii nzima tunawajibika kuwasimamia na kuwalea vizuri watoto wetu katika maadili yanayofaa kuanzia ngazi za familia,” alisema Mwenda,Alionya vijana dhidi ya vitendo viovu vinavyokiuka sheria na kuagiza Jeshi la Polisi wilayani humo kuendeleza misako kwa watakaokaidi maelekezo hayo. Alisema DC Mwenda
Aidha, aliwataka wazazi kuendelea kuwasisitiza vijana wao kushiriki kwenye shughuli za uzalishaji Malik ili kuepukana na vitendo vya udokozi na wizi wa vitu vidogovidogo.
Ziara hiyo iliambatana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, wakuu wa taasisi za umma na wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
Kwa upande wake, Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii, Mtaki Magina, alisisitiza wajibu wa jamii nzima katika malezi bora ya watoto na kuwataka wananchi kuachana na biashara haramu zisizokuwa na faida kwa jamii.
Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisimba Janson Mpenda,kwa niaba ya viongozi wenzake wa kijiji cha Kisimba, alimshukuru DC Mwenda kwa usikivu na utekelezaji wa ahadi zake katika kuleta maendeleo wilayani humo.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.