Vijiji 40 Kati ya vijiji 70 Wilaya ya Iramba Mkoani Singida vinatarajiwa kunufaika na mradi wa uboreshaji na usalama wa milki za Ardhi ikiwemo upimaji mipaka, kutenga maeneo ya Malisho, Kilimo, Maeneo ya Taasisi za Serikali, ama upangaji na matumizi Bora ya ardhi ndani ya Vijiji hivyo na kupewa Milki za kimila, Lengo kuu ni kuondoa Migogoro ya Ardhi iliyopo.
Hayo yamejiri Wakati wa mafunzo ya wadau wa ardhi yaliyoandaliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mafunzo yaliyofanyika wilayani Iramba na kufunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Yusuph Mwenda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Omary Dendego.
Katika hotuba yake kwa wadau hao ambao iliwahusisha Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata,Viongozi wa Dini,Viongozi wa Kimila, Wafanyabiashara, Walemavu, Wakulima wakubwa na Wadogo pamoja na viongozi wa Taasisi za Serikali na Binafsi, Mkuu wa Wilaya Suleiman Mwenda anasema.
"Migogoro ya Ardhi ni Mingi katika Nchi yetu. Kwenye ziara ya Katibu Mwenezi Itikadi na Mafunzo CCM, katika ripoti yake, Zaidi ya asilimia 70 ya kero alizozitatua ni migogoro ya Ardhi ; Hivyo ilimfanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kugundua hili ni tatizo kubwa akakopa fedha Benki ya Dunia Dola Mil. 150 sawa na Bilioni 346, kwa ajili ya kupima na kutoa Hati milki za Kimila zaidi ya Milioni 2 nchini na ndiyo maana na Iramba imenufaika na Mil. 600". Amesema Mwenda.
"Ni Imani yangu baada ya kukamilika kwa zoezi hili Migogoro ya Ardhi Iramba na kote nchini itakuwa imepungua kamasiyo kuisha kabisa ". Ameongeza DC Mwenda
Katika Vijiji 40 ambavyo vinanufaika na mradi huu Wilayani Iramba ni pamoja na Kinalilya, Kisana, Kisimba, Kisiriri, Ulemo, Uwanza,Maluga,Galangala, Kyalosangi, Kisharita, Nguvumali, Mdonkolo, Zinziligi, Songambele, Luzilukulu, na Lunsanga.
Vingine ni Kisonga, Urughu, Kaselya, Nsonga, Kipuma, Ndulungu, Mwanduigembe, Mahola, Mang'ole, Mlandala,Masimba,Ujungu, Msai, Mtoa, Tintigulu, Wembere, Kibigiri, Mingela, Nsunsu, Luono,Ndurumo, Kidaru, Msansao na Tyegelo
Aidha Vijiji ambavyo tayari Vimeshapimwa na Kuingia kwenye matumizi Bora ya Ardhi ni pamoja na Kisimba, Kisiriri, Kinalilya, Kisana, Kyalosangi, Uwanza, Kisharita, Galangala, Ulemo, Maluga, Zinziligi, Urughu, Kisonga, Kaselya, Luzilukulu, Lunsanga, Nguvumali, Nsonga, Songambele, na Mdonkolo Vijiji hivi Vimepitiwa kuanzia Februari 10 2024 hadi April 17,2024.
Vijiji ambavyo Mradi umeendelea navyo ni Kipuma, Ndulungu, Mwanduigembe, Mahola, Mang'ole, Mlandala, Masimba, Ujungu, Msai, Mtoa, Tintigulu, Wembere, Kibigiri, Mingela, Nsunsu, Luono, Ndurumo,Kidaru, Msansao na Tyegelo
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.