JUMLA YA TSHS M 411.939.ZIMEKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI YA KINAMBEU ULIOCHUKUWA TAKRIBANI MIAKA 12 ,MKUU WA WILAYA YA IRAMBA MKOANI SINGIDA SULEMAN MWENDA AELEZA
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida; Suleman Yusuph MWENDA,Amezindua Rasmi Zahanati ya Kinambeu iliyopo katika Kata ya Old-Kiomboi Wilayani Iramba Mkoani Singida ,iliyojengwa Kwa Awamu mbili Tofauti na kuchukuwa TAKRIBANI MIAKA 12 kukamilika ambpo Kwa mara ya kwanza ilianzishwa kujengwa Kwa nguvu za Wananchi Tangu Julay 25---2011.
Akiongea na Wananchi Wa kijiji Cha Kinambeu mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleman Yusuph Mwenda; Amesema Zahanati hiyo itatoa Huduma ya Afya Kwa Mama wajawazito na Watoto pia Jamii ya Iramba Kwa ujumla.
Aidha Mwenda Amewataka Wananchi hao kuitunza Zahanati hiyo Ili Iweze kudumu na kutoa Huduma njema Kwa Wananchi huku wakipanda miti na kutinza mazingira.
Kwa hatua nyingine Dc Mwenda Amempongeza Katibu Mkuu wa chama Cha Mapinduzi CCM ndg Daniel chongolo Kwa mchango wake wa m1 pamoja na mbunge wa Iramba Dr.Mwingulu kwa Mchango wa Tsh milioni 2 lakini Kwa kuiagiza Serikali kuu kuleta Tsh M200 kumalizia jengo.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iramba Innocent Said Msengi Amesema mpaka Sasa Iramba inapaa Kwa kuwa na Zahanati 51 kati ya Vijiji 70 na kubakia Zahanati 19 kukamilisha kila kijiji kuwa na Zahanati yake.
Awali akisoma Taarifa Kwa Mgeni Rasmi kaimu Mganga mkuu w Wilaya ya Iramba Timothy Sumbe Amesema Zahanati hiyo ilianza na tsh Milioni 7.069 nguvu za Wananchi na kupata Muhisani Kwa ubalozi wa Japani aliyetoa Tsh Milioni 158.858.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.