Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Shirika la viwango Tanzania (tbs) limeendesha Semina kwa wazalishaji na wasindikaji wa bidhaa ya mafuta ya kula wilayani Iramba.
Semina hiyo imefanyika leo Alhamisi Frebuari 20, 2020 Ukumbi Mdogo wa Halmsahuri mjini hapa.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Makwaya amewataka wajasiriamali na wasindikaji wa mafuta kufahamu kua mafunzo hayo yakitekelezwa ni fursa muhimu inayochangia pato la Taifa, kuongeza ajira na kuondoa umasikini inchini.
Mafunzo hayo yatawawezesha kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya viwango na kuziongezea thamani bidhaa zinazozalishwa kupitia mfumo wa uthibitishaji ubora wa bithaa.
Kuyaingiza mafuzo hayo kivitendo kutaiwezesha serikali kufikia malengo ya Taifa ifikapo 2025 kua na uchumi wenye nguvu, imara na wenye ushindani.
Aidha Makwaya amewataka washiriki hao kuelewa lengo la mafunzo hayo kua ni kujipatia elimu juu ya viwango, uthibitishaji ubora wa bidhaa na usajili wa jengo, teknolojia za usindikaji wa mafuta ya kula, usajili wa biashara, usafi katika maeneo ya uzalishaji kama vile hotel, migahawa na maeneo mengine yanayohusiana na chakula na vipodozi.
“ Mnapaswa kufahamu kua serikali inahitaji ushiriki wenu katika vita ya umasikini ili kutekeleza hayo na hatimaye kufanikisha malengo ya kuifanya Tanzania kua nchi ya viwanda,” amesisitiza Makwaya
Kwa upande wake Meneja wa Utafiti na Mafunzo wa Shirika la Viwango Tanzania (tbs), Mwl. Hamisi Mwanasala amewaagiza Wajasiriamali hao kuongeza thamani bidhaa zao ili waweze kuuza ndani na nje ya nchi.
Pia amewataka kua mabalozi kuwafikishia elimu wajasiriamali ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuria mafunzo hayo.
Naye Afisa viwango kutoka katika Shirika hilo, Zena Issa amewaagiza kuhakikisha kua bidhaa zao zinakua na brand au maelekezo muhimu yanapatikana kwenye kifungashio cha bidha hizo.
Halikadhalika amewakumbusha kua ufahamu wa watumiaji au walaji nchini umekua mkubwa kiasi kwamba huwa waangalifu wakati wa kununua bidhaa ili kupata bidhaa zilizothibitishwa ubora wake.
Aidha amewataka wajasiriamali kote nchini kuhakikisha bidhaa zao zinakidhi ubora kulingana na kiwango husika na zimethibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (tbs) ili kuweza kutumia fursa ya soko la ndani na hata lile la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Katika mafunzo hayo Wajasiriamali wamejifunza mada ya viwango, matumizi na faida zake, utaratibu wa kupata leseni ya alama ya ubora wa bidhaa na usajili wa majengo, usafi wa maeneo ya kuuzia bidhaa za mafuta yakula, teknolojia za usindikaji bidhaa za mafuta ya kula, kanuni bora za uzalishaji na uhifadhi wa mafuta ya kula, utaratibu wa kufuata wakati wa urasimishaji wa biashara na huduma zitololewazo na ofisi maendeleo ya jamii.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Emmanuel Makwaya akiwa na wataalamu mbalimbali waliowasilisha mada kwa wazalishaji na wasindikaji wa bidhaa ya mafuta ya kula katika semina ya Shirika la viwango Tanzania (tbs) wilayani Iramba. Picha na Hemedi Munga
Baadhi ya wazalishaji na wasindikaji wa bidhaa ya mafuta ya kula wakiwa katika semina ya Shirika la viwango Tanzania (tbs) wilayani Iramba. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.