Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, B’hango Lyangwa amezindua mashindano ya umitashumta Wilayani Iramba.
Lyangwa amezindua mashindano hayo leo Ijumaa Februari 21, 2020 katika uwanja wa shule ya Msingi Kiomboi Bomani mjini hapa.
Amewahamasisha wanafunzi kua wanapaswa kuzingatia michezo kwa kua michezo inajenga afya, ushirikiano na fursa inayoleta ajira.
Pia amewataka kua na nidhamu pindi wawapo ndani ya uwanja ili wasiweze kuumizana na hata wanapo kua nje ya uwanja.
Aidha ametumia nafasi hiyo kuwapongeza Walimu kwa uvumilivu mkubwa walionao wa kuwalea wanafunzi hao kimaadili, nidhamu na kimichezo.
Wanafunzi hao wakilelewa kwa nidhamu hiyo ni wazi kua watapatikana wachezaji wazuri na mwisho kua na timu nzuri itakayoweza kuitangaza Iramba kitaifa.
Kupitia kauli mbiu ya mwaka 2020 inayosema “Hongera Awamu ya Tano kuenzi sanaa, taaluma na michezo, 2020 chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu,"
Lyangwa ameitaka hadhira iliyohuzuria uzinduzi huo kuienzi serikali ya Awamu ya Tano kwa sababu inathamini na kuendeleza michezo.
Awali akitoa taarifa fupi ya uzinduzi wa mashindano ya michezo na taaluma kwa shule za msingi Tanzania, Afisa Utamaduni wa Wilaya hiyo, John Kitto amesema uzinduzi utahusisha michezo mbalimbali itakayofanyika katika shule zote zilizopo Wilaya Iramba.
Ingawa kiwilaya uzinduzi unafanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kiomboi Bomani kwa kushirikisha shule tano zinazowakilisha shule zote zilizopo katika Halmashari.
Kitto amezitaja shule hizo, kua zipo zilizotengwa kanda A ambapo inajumuisha shule ya msingi Igumo, Kiomboi Bomani na Kizega.
Wakati kanda B inajumuisha shule ya msingi Lulumba na Salala.
Kufuatia uzinduzi huo, michezo anuai ilichezwa kwa kushirikisha kanda A na kanda B.
Ambapo mchezo wa mpira wa miguu uliowakutanisha kati ya Kanda A na kanda B kwa upande wa wavulana na kusakata kandanda safi lililoifanya kanda A kuibuka na Ushuindi mwembamba wa bao moja bila dhidi ya kanda B.
Nao upande wa wasichana kati ya kanda A na kada B kwa mpira wa miguu uliopigwa katika kiwanja hicho na kuufanya mchezo huo kuisha bila ya kufungana.
Kwa upande wa mchezo wa netball uliotimua vumbi katika kiwanja hicho, mpaka dakika zinakamila ni Kanda B walioibuka na ushindi wa mabao 13 dhidi ya Kanda A.
Uzinduzi huo pia ulihusisha mchezo wa kuvuta kamba, mpira wa wavu, kukimbia riyadha na uimbaji wa kwaya.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, B’hango Lyangwa akimpigia mpira kipa wa timu ya Walimu kuashiria uzinduzi wa mashindano ya umitashumta Wilayani Iramba. Picha na Hemedi Munga
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, B’hango Lyangwa akimpigia mpira kipa wa timu ya Wanafunzi kuashiria uzinduzi wa mashindano ya umitashumta Wilayani Iramba. Picha na Hemedi Munga
Afisa Utamaduni wa Wilaya ya Iramba, John Kitto akitoa taarifa fupi ya uzinduzi wa mashindano ya michezo na taaluma kwa shule za msingi zilizopo Iramba. Picha na Hemedi Munga
Wanafunzi mbalimbali wakiwa katika uwanja wa shule ya msingi Kiomboi Bomani wakiendelea na mchezo wa wavu. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.