Kamati ya fedha, Mipango na Utawala wilaya ya Iramba ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mhe: Simion Tyosera (Diwani wa CCM kata ya Urughu) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni na Wakuu wa Idara na Vitengo wamefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani Iramba
Ziara ya ukaguzi wa hatua ya ujenzi wa miundombinu katika miradi mbali mbali ya maendeleo ndani ya wilaya ya Iramba imefanyika leo katika maeneo yaliyoshirikisha ujenzi wa miradi hiyo ya maendeleo kwa jamii.
Ziara hiyo iliongozwa na jopo la Kamati ya Wilaya ya Fedha, Mipango na Utawala wilayani Iramba inayoundwa na waheshimiwa Madiwani wa kata mbali mbali wilayani humo.
Katika ziara hiyo kamati ya Wilaya ya Fedha, Mipango na Utawala imefanya ukaguzi katika Ujenzi wa miradi ya maendeleo ya Ujenzi hosteli ya shule ya sekondari Kinambeu, Ujenzi wa stendi ya magari makubwa Misigiri na chuo cha ufundi stadi (VETA) kwa lengo la kuwawezeha vijana wanaotoka katika maeneo ya vijijini ili waweze kujifunza fani mbalimbali ambazo zitawasaidia kupata ujuzi na kuanzisha viwanda vidogovidogo na kujiajiri wao wenyewe.
Jopo hilo la Madiwani ambao pia ndiyo kamati ya fedha, Mipango na Utawala ya Wilaya ilipongeza hatua ya Ujenzi iliyofikiwa katika miradi hiyo huku wakiendelea kusisitiza madiwani wa kata husika watendaji, wenyekiti wa vijiji na vitongoji kuhakikisha kwamba wanashirikiana kwa pamoja na wananchi wao kukamilisha miradi hiyo katika muda pangwa.
Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala imeongeza kusema kwamba inatambua vyema nguvu za wananchi wa maeneo hayo katika kufanikisha Ujenzi wa miradi hiyo ya maendeleo hadi kufikia hapo ilipo sasa na kusema ni hatua kubwa waliyoichukua ya kujitambua na kuhakikisha wanashirikiana na serikali ya awamu ya tano
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.