Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Simion Tyosela amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Linno Mwageni kuongeza kasi ya ujenzi wa stendi mpya ya mabasi ya Misigiri inayojengwa kijiji cha Misigiri kata ya Ulemo.
Tyosela ametoa agizo hilo leo Alhamisi Machi 5, 2020 wakati walipofanya ziara katika eneo hilo akiwa na Kamati ya Fedha Mipango na Utawala ya Halmashauri hiyo.
Katika ziara hiyo ameagiza kasi ya ujenzi iongezeke huku akiitaka kamati ndogo ya Ujenzi kuhakikisha barabara ya kuchepuka wakati wa kuingia na kutoka katika stendi hiyo inakamila mara moja.
“Ninaagiza kasi ya ujenzi iongezeke na kuhakikisha barabara za mchepuko zinakamila kwa wakati,”amesisitiza Tyosela
Akisoma taarifa ya ujenzi wa stendi hiyo, Mchumi wa Halmashuri, Mapenzi Lenjima amesema takribani Tshs11.81 milioni zimekisiwa kukamilisha ujenzi huo.
Amefafanua kuwa mpaka sasa ujenzi umefika hatua ya lenta ambapo Tshs5.9 milioni zimetumika kujenga choo chenye matundu matatu ya wanaume na matundu matano ya wanawake.
Pia amewakumbusha waliopewa vibanda kulipa Tshs 50,000 ili kukamilisha ujenzi kwa wakati huku akiwatahadharisha wale watakaoshindwa kulipia kuwa vibanda watapewa waliokuwa tayari kulipia.
Aidha amesema wanatarajia kujenga jengo la kupumzikia abiria na kibada cha polisi.
Kamati ya Fedha Mipango na Utawala ya Halmashuri hiyo imeendelea na ziara mpaka kijiji cha Nselembwe kata ya Shelui eneo ambalo litajengwa kituo cha Afya.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Hussein Sepoko ameishukuru serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuleta Tshs400 milioni za ujenzi wa kituo hicho.
Sepoko amesema kuwa majengo matano yanatarajiwa kujengwa ambayo ni jengo la mama na mtoto, jengo la upasuaji (theater), nyumba ya mtumishi, jengo la kufulia (laundry), jengo la kuhifadhia maiti(mortuary) na jengo la maabara (laboratory).
Katika ziara hiyo wajumbe wa kamati hiyo walipata fursa yakutoa mapendekezo mbalimbali.
Diwani wa kata ya Ntwike, Albert Makwala aliishauri kamati ya ujezi wa kituo hicho kuchukua tahadhari ya mkondo wamaji unaopita katika eneo hilo huku akiitaka kamati hiyo kutegemea ushauri wa kitaalamu.
Naye Diwani wa kata ya Kyengege Innocent Msengi aliitaka kamati hiyo kuongeza kasi ya ujenzi wa kituo cha Afya nakuhakikisha kutokuwa na madoa doa.
Halikadhalika amewataka waungane ili wafanye mabadiliko ya haraka kwa kuwa fedha wanazo.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Samwel Shillah ameuagiza uwongozi wa kata ya Shelui kupanda miti katika mipaka ya eneo hilo na kuhakikisha barabara zinatengenezwa vizuri na kuacha lango kuu la kuingilia kituoni hapo linakua moja.
Ziara ya Kamati ya Fedha Mipango na Utawala imetembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa stendi mpya ya mabasi ya Misigiri inayojengwa kijiji cha Misigiri kata ya Ulemo, mradi wa kituo cha Afya utakojengwa kijiji cha Nselembwe kata ya Shelui na mradi wa nyumba ya Walimu, bweni la wanafunzi na bwalo la wanafunzi vinavyojengwa katika shule ya sekondari Shelui.
Kamati ya Fedha Mipango na Utawala ya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ikikagua eneo la kijiji cha Nselembwe kata ya Shelui ambalo litajengwa kituo cha Afya kwa fedha zilizoletwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Picha na Hemedi Munga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni akiwaonesha baadhi ya wakuu wa Idara wa Halmasghauri hiyo eneo la kijiji cha Nselembwe kata ya Shelui ambalo litajengwa kituo cha Afya kwa fedha zilizoletwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Picha na Hemedi Munga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni akiwa na baadhi ya wakuu wa Idara wakati wa kukagua eneo la kijiji cha Nselembwe kata ya Shelui ambalo litajengwa kituo cha Afya kwa fedha zilizoletwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Picha na Hemedi Munga
Mwandishi wa vikao vya Halmashauri, Ndugu Neema akiwa na Diwani wa kata ya shelui katikati, Kinota Hamisi na kulia mwa Diwani huyo ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Samwel Shillah. Picha na Hemedi Munga
Mradi wa nyumba ya walimu unaojengwa shule ya sekondari Shelui. Picha na Hemedi Munga
Mradi wa bweni unaojengwa shule ya sekondari Shelui. Picha na Hemedi Munga
Afisa Elimu sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Godfrey Mwanjala akionesha jambo wakati wa ukaguzi wa Kamati ya Fedha Mipango na Utawala shule ya sekondari ya Shelui. Picha na Hemedi Munga
Mradi wa bwalo unaojengwa shule ya sekondari Shelui. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.