Kamati ya fedha,Mipango na utawala ya Halmashauri wilaya ya Iramba imeeleza kuridhishwa kwake na ubunifu uliotumika katika kutekeleza miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kupitia mradi wa BOOST na ile iliyotekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mhe. Innocent Msengi ameeleza kuridhishwa na hali ya utekeleza wa miradi hiyo baada ya kukamilika kwa ziara iliyofanyika Julai 24, 2023 ambapo miradi mbalimbali ikiwemo y, Elimu, Utawala na Afya iliweza kutembelewa na kukaguliwa.
Mhe. Msengi ametoa pongezi kwa walimu wakuu na wakuu wa shule,watendaji wa kata na Wataalamu wa idara ya Afya walioonesha ubunifu katika miradi hiyo na kuwataka watekelezaji wengine kuiga mfano huo ambao ameuita ni wa Kizalendo, na kumtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba, kukaa na wataalamu ili kurekebisha kasoro zilizobainika katika miradi michache ikiwemo ya elimu na afya ili miradi iweze kukamilika na wananchi kunufaika nayo.
Aidha Mhe.Innocent Msengi ameipongeza Serekali ya awamu ya sita kwa kuona umuhimu wa kujenga Shule za msingi kupitia Mradi wa BOOST nakusema kuwa ujenzi huo utakapokamilika wananchi watanufaika nao kwa upande wa elimu na kupunguza Adha ya wanafunzi kutembea umbali kwa ajili ya kupata elimu.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii Mhe. Peter John Peter, akizungumzia ziara hiyo amesema ni utaratibu wa kawaida ambao unaboresha utendaji kazi wa watumishi katika halmashauri ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kuwapongeza wasimamizi wa miradi katika shule ya Msingi Kibululu,Ishanga,Zahanati ya Kinambeu kwa kusimamia vizuri miradi na kuwa wabunifu hali iliyofanya thamani halisi ya fedha kuonekana katika utekelezaji wa Mradi hiyo.
Kwa upande Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwalimu Godfrey Mwanjala amewapongeza walimu,watendaji wa kata na Vijiji na wataalamu mbalimbali kwa usimamizi mzuri wa miradi ya BOOST na ile ya Serikali Kuu na kuwaasa watekelezaji wengine wa miradi inayoendelea na itakayokuja kuiga mfano mzuri wa walimu katika kusimamia miradi.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.