Hemedi Munga. Irambadc
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi ameishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt, John Magufuli ambayo imeendelea kuleta fedha za miradi ya maendeleo Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Msengi ameyasema hayo leo Alhamisi Januari 21, 2021 wakati akiwa na kamati ya Fedha, Mipango na Utawala wa Halmashauri hiyo, Tumaini Sekondari kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani hapo.
Amewaagiza wataalamu na kamati mbalimbali za ujenzi wa miradi hiyo kuingiza nguvu za wananchi katika taarifa zao ili kuonesha namna ambavyo wanaiunga serikali mkono katika kuwaletea Wananchi maendeleo.
Katika hatua nyingine, Msengi amewataka Walimu Wakuu na Wakuu wa shule zote Wilayani humo kuhakikisha wanafunzi wote wanaostahili kwenda shule wemefika na kuanza masomo.
Akihoji mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala kuhusu kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati, Peter John amesema muda uliobakia ni mchache je miradi hii itakamilika kwa wakati uliopangwa.
Akijibu hoja ya mjumbe wa kamati ya fedha, Mipango na Utawala mmoja wa wataalamu wanaosimamia miradi ya shule ya Msingi Bomani kunakojengwa madarasa mawili, Hassan Mwanga amesema kuwa miradi hiyo itakamilika kwa wakati kwa kuwa fedha na malighafi vya kumalizia vipo na kwa kuzingatia mikataba ya mafundi inayowataka wamalize kabla ya januari 31, mwaka huu.
Kwa upande wake mjumbe wa Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala, Jenifer Miano ameziomba kamati za ujenzi wa miradi hiyo kuongeza kasi, usimamizi wa dhati na wenye ufanisi ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kiwango stahiki.
Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala ya Halmashauri hiyo, imetembelea baadhi ya miradi yenye takribani Tsh 1.6 bilioni.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi Kiomboi Bomani, ujenzi wa hostel shule ya sekondari Lulumba, ukarabati na ujenzi wa miundombinu mbalimbali shule ya sekondari Tumaini, ujenzi wa kituo cha afya Shelui, ujenzi wa stendi ya Misigiri na ujenzi wa madarasa matatu shule ya msingi Kyengege.
Mwisho
Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala ikiwa mbele ya moja ya jengo la Kituo cha Afya Shelui Wilayani Iramba ,Mkoa wa Singida wakisikiliza taarifa ya ujenzi wa kituo hicho baada ya kutembelea na kukagua ujenzi huo. Picha na Hemedi Munga
Hatua ya ujenzi wa Hosteli shule ya sekondari Lulumba ilipofikia siku chache ilipotembelewa na kukaguliwa na Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala. Picha na Daudi Mujungu
Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala wakiwa katika viwanja vya Lulumba Sekondari wakisikiliza taarifa ya ujenzi wa Hosteli baada ya kutembelea na kukagua ujenzi huo. Picha na Daudi Mujungu
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.