Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Iramba imefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali kwa robo ya Pili Mwaka wa fedha 2024/2025.
Ziara hiyo imefanyika Januari 23, 2025 kwa kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa Ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa, Matundu 6 ya Vyoo vya wanafunzi Shule ya Msingi Tyeme kupitia Mradi wa BOOST (Mil. 127,200,000), ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari inayojengwa Kata ya Mtoa Kupitia Mradi wa SEQIP (Mil. 544,225,626), Mradi wa Ujenzi wa vyumba Vinne vya madarasa, Mabweni 2 na matundu 12 ya Vyoo kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano Shule na Sekondari Kinambeu (Mil. 362,000,000), Ujenzi wa nyumba ya walimu mbili kwa Moja Shule ya Sekondari Iramba (Mil. 95,000,000)na ujenzi wa Shule mpya ya Amali iliyopo Kijiji Cha Kitukutu (Bil. 1,600,000,000).
Akitoa majumuisho ya ziara hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mhe. Innocent Msengi amepongeza hatua za ujenzi shule ya Msingi Tyeme, shule ya Sekondari Kinambeu, ujenzi wa vyumba ya mwalimu shule ya Sekondari Iramba na kusisitiza kuongeza kasi ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Mtoa na Shule mpya ya Amali.
Pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Wilaya ya Iramba fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Na amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba na viongozi wengine kwa kuendelea kuwatumikia Wananchi wa Wilaya ya Iramba.
"Kwanza namshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Kuleta fedha kwa Halmashauri yetu na pia Mkurugenzi Mtendaji kwa utekekelezaji wa miradi hii, rai yangu usimamizi uendelee kufanyike ili iishe kwa muda uliopangwa". Alisisitiza Mhe. Msengi.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.