Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara, na Mazingira Mhe Ahmed Sadddiq Suleiman (Mb), akiwa na Makamu Mwenyekiti Mhe: Innocent Bashungwa (Mb), Naibu waziri wa Muungano na Mazingira Mhe: Kangi Alphaxard Lugola (Mb), Mhe: Balozi Dkt. Diodorus Buberwa Kamala (Mb), Mhe: Kanali (Mst)Masoud ali Khamis (Mb), Mhe: Musa Rashid Ntimizi (Mb), Mhe: Khamis Ali vuai (Mb),Mhe: Munira Mustafa Khatibu (Mb), Mhe: Gimbi Dotto. Masaba (Mb), Mhe: JosephineJohnson Genzabuke (Mb), Mhe: Omary Ahmad Badwel (Mb), Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe: Emmanuel Luhahula, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe: Simion Tiyosera, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Iramba Wakili: Boniface Engelberth Kalikona na Viongozi Mbalimbali wamefanya Ziara ya kukagua Machimbo ya Dhahabu Nkonkilangi Wilaya ya Iramba Mkoani Singida
Katika Ziara hiyo, Wamefanya Mkutano wa hadhara na Wachimbaji wadogo wadogo wa Dhahabu Nkonkilangi Wilaya ya Iramba Mkoani Singida ili kujua changamoto wanazozipata kwenye shughuli zao za Uchimbaji zikiwemo vifaa duni vya kutolea mawe ndani ya Mashimo pamoja na Vifaa vya Kuchenjua Dhahabu.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira amewahimiza Wanchimbaji kujitegemea ili waweze kuingia kwenye uchumi wa Kati ili kuunga juhudi za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Dkt. John Joseph Magufuli.
Vile vile amesistiza utunzaji wa Mazingira ni wajibuwa kila mmoja kuhakikisha Mazingira yanakuwa salama na kuwaomba viongozi wote kuongeza kasi ya kusimamia Sheria ya mazingira kwa wale ambao hawasimamii, sheria ichuke mkondo wake na sio tu kwenye migodi bali pia kwenye Viwanda.
Aidha amewapongeza Sana kwa hatua wanazozitekeleza kama wachimbaji wadogowadogo na kuwaahidi kutatua changamoto ambazo zipo nje ya uwezo wao kama Umeme, Pump ya kuvuta maji ndani ya Mashimo pamoja na kupewa Mikopo.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Mhe:Emmanuel Luhahula akiwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakikagua Maduara ya Machimbo ya Dhahabu Nkonkilangi Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.