Kamati ya Mipango na fedha ya Wilaya ya Iramba imeambatana na Kaimu Mkurugenzi Ndg.Emmanuel Makwaya na Wakuu wa Idara na Vitengo wamefanya Ziara ya Kukagua Miradi ya Maendeleo Wilayani Iramba
Ziara ya ukaguzi wa hatua ya ujenzi wa Miundombinu katika miradi ya mbali mbali ya maendeleo ndani ya Wilaya ya Iramba imefanyika leo katika maeneo yaliyoshirikisha ujenzi wa Miradi hiyo ya Maendeleo kwa jamii.
Ziara hiyo iliongozwa na jopo la Kamati ya Wilaya ya Mipango na Fedha wilayani Iramba inayoundwa na waheshimiwa Madiwani wa Kata mbali mbali Wilayani humo.
Katika ziara hiyo kamati ya Wilaya ya Mipango na Fedha imefanya ukaguzi katika Ujenzi wa miradi Maendeleo ya Ujenzi wa shule ya Kugulusungi Kata ya Mtekente na Shule Shikizi ya Ulyang’ombe Kijiji cha Makunda Kata ya Kyengege, miradi mingine ni Kituo cha Afya Ndago pamoja na Kituo cha Afya cha Kinampanda.
Jopo hilo la Madiwani ambao pia ndiyo kamati ya Mipango na Fedha ya Wilaya ilipongeza hatua ya Ujenzi iliyofikiwa katika miradi hiyo huku wakiendelea kusisitiza madiwani wa kata husika watendaji, wenyekiti wa vijiji na vitongoji kuhakikisha kwamba wanashirikiana kwa pamoja na wananchi wao kukamilisha miradi hiyo katika muda pangwa.
Kamati ya Mipango na Fedha imeongeza kusema kwamba inatambua vyema nguvu za wananchi wa maeneo hayo katika kufanikisha Ujenzi wa Miradi hiyo ya maendeleo hadi kufikia hapo ilipo sasa na kusema ni hatua kubwa waliyoichukua ya kujitambua na kuhakikisha wanashirikiana na serikali ya awamu ya tano.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.