Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Iramba imetoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa Skimu ya Umwagiliaji Masimba ambayo ujenzi wake tayari umeanza na unatarajiwa kuwanufaisha Wakulima zaidi ya 24000
Pongezi hizo zimetolewa Jumatatu Machi 10,2025 na Kamati hiyo inayongozwa na Mwenyekiti wake, Ndg. Samuel Joel Asher, wakati kamati hiyo ilipokagua na kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa Wilayani Iramba.
Katika ziara hiyo, Kamati ilikagua miradi ya maendeleo ikiwemo Skimu ya Umwagiliaji Masimba,Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu (2 kwa 1) Shule ya Msingi Ushora Utemini yenye thamani ya Milioni 95 kupitia Programu ya GPE- TSP (Teachers Support Program), ambapo Hatua za Awali kwa ajili ya kuanza ujenzi zimeanza, Ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Makunda kupitia Mradi wa Sequip kwa Gharama ya Milioni 544,225,626.
Katika ziara hiyo, Kamati pia ilitembelea Shule ya Msingi Msansao ili kujionea Mazingira ya utoaji wa Elimu shuleni hapo ikiwa imeendelea kufanya vizuri katika taaluma ambapo kwa upande wa mtihani wa kumaliza Elimu ya msingi, asilimia ya ufaulu imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka ambapo kwa miaka mitatu mfululizo ufaulu umepanda kutoka asilimia 25 ya mwaka 2021 hadi asilimia 74 mwaka 2024.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.