KAMATI YA USHAURI YA WILAYA DCC YAJADILI MAPENDEKEZO YA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026
Kamati ya ushauri ya Wilaya ya Iramba DCC, imejadili na kupitisha mapendekezo ya rasimu ya mpango wa bajeti yenye jumla ya kiasi cha Shilingi 38,088,278,131.59 kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Akifungua kikao hicho Machi 5,2025 katika ukumbi mkubwa wa mikutano Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda amesema lengo la kikao hicho ni kujadili taarifa mbalimbali za utendaji kazi wa Halmashauri kwa ujumla pamoja na kupitisha mapendekezo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Kikao kimehudhuriwa pia na Katibu Tawala Wilaya,Mwenyekiti wa Halmashauri,Kaimu Mkurugenzi,Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo,Viongozi mbalimbali wa Dini, Viongozi wa Vyama Vya Siasa na Wataalamu mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya Iramba.
Katika Kikao hicho , Rasimu ya mapendekezo ya Bajeti imewasilishwa na Kaimu Afisa Mipango na Uratibu Bi. Geni Madaha Megeli kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri.
Bi. Geni Megeli alifafanua kuwa Halmashauri inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya Tsh.38,088,278,131.59 kwa ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo na kutoa mchanganuo wa fedha hizo zinazokadiriwa katika Bajeti hiyo kuwa kiasi cha shilingi 21,824,464,000.00 ni fedha ya mishahara ya Watumishi, Kiasi cha Shilingi 2,443,743,000.00 ni matumizi ya kawaida (OC), Kiasi cha Shilingi 2,062,726,000.00 ni Ruzuku ya miradi ya maendeleo, Kiasi cha Shilingi 5,083,457,252.00 ni fedha kutoka kwa wahisani/wadau wa maendeleo na Shilingi ni 5,234,842,879.59 fedha zitokanazo na vyanzo vya Mapato ya ndani ya Halmashauri.
Wajumbe wa kamati wamepata nafasi ya kupitia,kujadili na hatimaye kwa kauli moja wameridhia kupitisha rasimu hiyo ya bajeti kwenda katika ngazi nyingine.
Mwenyekiti wa kikao ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba ametamatisha kwa kuwashukuru wajumbe wote kwa kushiriki na kuwapongeza kwa mawazo yao mazuri ya kujenga.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.