Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa. Kitila Mkumbo amefanya ziara ya kukagua uchimbaji wa visima vya maji kata ya Mgongo tarafa ya Shelui wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo ameongozana na Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe: Emmanuel Luhahula, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mhe: Simion Tyosera (Diwani wa CCM kata ya Urughu), Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Bi. Marietha Kasongo, Katibu tawala wilaya ya Iramba Ndg. Pius Songoma, waandisi wa maji ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida, waandisi wa maji wa wilaya ya Iramba na wataalamu mbalimbali katika ziara ya kukagua mradi wa uchimbaji wa visima kata ya Mgongo tarafa ya Shelui wilayani Iramba.
Akizungumza na kamati ya maji, Profesa kitila amemwaagiza mkandarasi pamoja na wataalamu wote wanaoshiriki kutekeleza mradi huo wasiwe kikwazo cha mradi huo kutokamilika kwa wakati na kufanikisha lengo la kumaliza kero ya maji kwa wakazi wa Kiomboi.
“Visima hivi vinatarajiwa kulisha mji wa Kiomboi pamoja na vijiji ambavyo vitapitwa na mradi huu, Lengo la mradi ni kuwapatia wananchi huduma ya maji safi na salama pamoja na kuboresha Afya na kuinua shughuli za kiuchumi za Wananchi, jukumu la wananchi watoe ushirikiano katika kutunza miundo mbinu iliyopo alisema Profesa Kitila.
Aliongeza kusema “Mradi huu una awamu mbili, awamu ya kwanza ya uchimbaji visima ambavyo vinagharimu kiasi cha Shilingi million 300 na mkandarasi wake ni wakala wa serkali wa ujenzi wa mabwawa na uchimbaji wa visima (DDCA) ambayo ni taasisi ya serikali na msimamizi wa mradi ni kampuni ya Don consult ltd.
Awali mradi huu tulitarajia ukamilike mwezi Januari 2019 lakini nimetembelea hapa na nimepata Maelezo ya wataalamu sasa tutalazimika kuongeza muda hadi Machi 2019 kutokana na Jiolojia walioikuta wataalamu katika uchimbaji wa visima, hata hivyo nimewaagiza kwamba wahakikishe mradi huu unakamilika mapema kwa sababu hii ni awamu ya kwanza tu na wamu ya pili ni mradi ambao utasanifiwa kwa ajili ya kusambaza maji kwa ajili ya kuelekea mji wa Kiomboi na vijiji ambavyo vitapitwa na mradi huu Alisisitiza Profesa Kitila.
Aidha Mradi wa pili utagharimu kiasi cha Shilingi bilioni 9 hadi billion 12, sasa hii awamu ya pili ndiyo kubwa lakini utekelezwaji wake unategemea kukamilika kwa mradi huu wa wamu ya kwanza na ilikuwa muhimu sana tufike hapa tuweze kutia msukumo, tunashukuru kwamba awamu ya kwanza ya uchimbaji wa kisima hiki kinaonesha kuna maji mengi, wataalam wameona kwamba maji ni ya kutosha takribani lita elfu 80 hadi laki 1 kwa saa ambayo yanatosha na ni mengi, tunarajia watakapopima yatakuwa maeneo haya na mpaka sasa wamechimba mita 106, lengo lilikuwa ni kufika mita 150 nadhani haitafika nadhani maji yameisha patikana alisema Profesa Kitila.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.