Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kwa kupata HATI SAFI kwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali mwaka 2018/2019 iliyosomwa katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo kujibu maagizo ya CAG.
Pongezi hizo, zimetolewa leo Juni 5, 2020 na Dkt. Lutambi wakati alipokua akiongea katika Baraza la Madiwani wa Halmashuri hiyo Ukumbi Mkubwa mjini hapa.
“Mhe, Mwenyekiti ninaomba niwapongeze Watendaji wenzangu maana tunaanza kuona dalili njema za ujibuji wa hoja, sasa tunaona idadi kubwa ya hoja zimefungwa,” amesema Lutambi na kuongeza
“Niwaombe wakati tunapitia hoja hizi ambazo hazijafungwa bado kunaonekana zipo hoja ambazo zinawezekana kufutika kabla ukaguzi unaofuata, hivyo tutumie fursa hii ili hoja ziendelee kufutwa na kuifanya Halmashauri kutokua na hoja tena.”
Akiongelea swala la kukaimu nafasi mbalimbali katika utumishi wa umma, ameawataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa mpaka watakapo fikia uandamizi hapo watakua na sifa ya kuwa Wakuu wa Idara.
“Niwaombe Watumishi wenzangu kukaimu kwako Idara kunakuongezea fusra ya kujifunza zaidi na kuwapa nafasi wengine kukupima kama kweli unafaa nafasi husika pindi utakapokua umefikia vigezo,”
“Niwahimize Watumishi wenzangu ambao bado mnakaimu kuendelea kuchapa kazi kwa bidii na weledi zaidi ili mwishoni muweze kapata nafasi hizo.” ametilia mkazo
Pia, amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Linno Mwageni kuhakikisha anachukua hatua mara moja kufuta hoja ya vitabu vinavyodaiwa kuwa na takriban Tsh 64.6milioni hazijaingia Serikalini.
“Ninaelekeza baada ya wiki mbili nione mabadiliko katika hoja hiyo, hatua zichukuliwe mara moja ili hao wanaodaiwa warudishe fedha za Serikali,” ameagiza Lutambi
Mapema akiwasilisha taarifa ya Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019, Kaimu Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo, Hadhiri Ngayunga amesema Halmashauri imepata Hati Safi kwa kuwa hesabu za Halmashauri kwa mwaka huo ziliandaliwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya Hesabu za Sekta za Umma.
Ngayunga amesema kwa mwaka 2020 juni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alitoa jumla ya hoja 95 zinazotakiwa kutekelezwa.
Amefafanua kuwa utekelezaji wa kufuta hoja hizo kabla ya ukaguzi wa mwaka 2019/2020 unaendelea kwa kasi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Simion Tyosela amesema mwaka 2016/2017 Halmashauri ilipata Hati yenye mashaka, hivyo iliwafanya waweze kutafakari na kufuata maelekezo ya CAG yaliyoiwezesha Halmashauri mwaka,2017/2018 na 2018/2019 kupata Hati Safi.
“Tumeibeba ilani ya Chama Cha Mapinduzi Vizuri kwa kutekeleza shughuli zote za kijamii vizuri, hivyo kutupa fusra kwa Rais wetu, Dkt. John Magufuli, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Mwigulu Nchemba na Madiwani wote tukienda kwa jamii yetu na kuwaomba watuongezee muda kwa sababu yale waliyokuwa wakiyatarajia tumeyatekeleza, hivyo kuondoa maswali kwa wagombea uchaguzi ujao,” amesema Tyosela na kushangilia kuwa
“Standadi geji mmeiona! ndio, Rea mmeiona ! ndio, Ndege mmeziona ! ndio, Stiglazi goji mmeiona ! ndio, kwa hiyo tulichopungukiwa ni muda tu tumalizie yote.”
Naye Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa Singida, Raphael Stone ameishauri Halmashauri hiyo kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato kwa sababu uchache wa mapato unaweza irudisha Halmashauri katika hali ya zamani kabla ya kupata Hati Safi mfululizo.
Pia, ameipongeza Halmashauri hiyo kwa namna wanavyojibu hoja kwa ufasaha huku akiwataka kuandaa nyaraka mbalimbali kwa ajili ya ukaguzi wa Hesabu za Serikalia kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
MWISHO
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Simion Tyosela akimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Linno Mwageni kutekeleza maagizo yote ambayo ameagiza kipindi ambacho Madiwani hawatokuepo. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula akiwaomba Madiwani wa Baraza hilo kuchukua hatua kali dhidi ya hoja ya tangu mwaka 2015/2016 kwa Watumishi wote waliohusika na uzalishaji wa hoja hiyo, huku akiwapongeza Madiwani na Wataalam hao kwa kupata Hati Safi mfululizo. Picha na Hemedi Munga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni akiahidi kuyafanyia kazi maagizo yote yaliotolewa na viongozi mbalimbali wakati wa Baraza maalum la kushughulikia maagizo ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali CAG. Picha na Hemedi Munga
Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Nje Mkoa wa Singida, Raphael Stone pamoja na Mkaguzi wa Nje, Zainab Julius wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa hoja mbalimbali zilizofutwa na ambazo zinaendelea kushughulikiwa Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakati wa kikao maalum cha kujibu maagizo ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG). Picha na Hemedi Munga
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Iramba, Ibrahim Mjanaheri akimpongeza Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa kuwapandisha Watumishi wawili kuwa Wakuu wa Idara Baraza la Madiwani lililopita huku akimuomba kuhakikisha makaimu wengine wa Idara na Vitengo mbalimbali wanapanda kwa sababu kupanda kuwa Mkuu wa Idara au Kitengo ni motisha kwao. Picha na Hemedi Munga
Baadhi ya Madiwani wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa hoja mbalimbali zilizofutwa na ambazo zinaendelea kushughulikiwa Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakati wa kikao maalum cha kujibu maagizo ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG). Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.