Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt Rehema Nchimbi ameungana na baraza la madiwani (fullcouncil) la Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kwenye ukumbi wa Halamshauri. Baraza hilo limeongozwa na Mweneyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba, Diwani wa CCM Kata ya Urughu Mhe. SimionTiyosera kujadili mambo mbalimbali.
Dkt. Nchimbia kizungumza kwenye braraza la madiwani, amepongeza Halmashauri ya wilaya ya Iramba kupata hati Safi.
Aidha Dkt. Nchimbi amewaomba watendaji wote kushirikiana na kuwa na mshikamano kwa ajili ya kutatua changamoto za Wananchi wa wilaya ya Iramba. Alisema watendaji wote wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba tusisubiri kuharibikiwa ili tulaumiane haisadii chochote.
Vilevile Dkt. Nchimbi aliwaomba watendaji wote wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba kusimamia vema uchimbaji wa Dhahabu, kilimo chazao la Pamba na ziwa Kitangiri ili vinufaishe wilaya ya Iramba.
Mkuu wa wilaya Mhe. Emanuel Luhahula akizungumza kwenye baraza la madiwani aliwaomba watendaji wote wa Halmashauri kufanya kazi kwa ushirikiano ili kutatua changamoto zilizopo kwenye wilaya ya Iramba.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Mhe.Simion Tiyosera akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani. Baadhi yamadiwani wa halmashauri ya wilaya ya Iramba wakifatilia mijadala kwenye kikaohicho.
Baadhi ya Madiwani wa wilaya ya Iramba wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iramba mkoa wa Singida.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni akizungumza katika kikao cha baraza la Madiwani wa Halamshauri.
Baadhi ya watendaji wa Halmashari ya wilaya ya Iramba wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Singida.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.