Halmashauri ya Wilaya ya Iramba imefanya kikao cha Kamati ya Lishe ili kujadili taarifa ya utekekelezaji wa Afua za Lishe kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 ambacho kimefanyika leo tarehe 07/11/2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Kikao hicho kimeongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri Ndug. Jeremia Kahurananga na kimeketi kujadili taarifa hiyo kwa Kitengo cha Huduma za Lishe, Idara ya Elimu ya awali na Msingi, Idara ya Elimu Sekondari, Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Divisheni ya Maendeleo ya Jamii pamoja na kitengo cha Tiba mbadala/Asili.
Akizungumza katika kiako hicho Kahurananga ametoa rai kwa wajumbe wa kikao kwenda kuyatekeleza yote yaliyojadiliwa katika kikao hicho ikiwa ni pamoja na kwenda kuwatembelea watoa huduma za lishe ili kufahamu changamoto zao na kuzitatua.
“Tulichokubaliana ni kwamba sasa tutoke, afua za lishe sio za kujadiliwa tu kwa muhtasari ya kikao kilichopita na hiki cha leo bali ni kwenda kujadiliana kwa kina yale amabayo tumekwenda kuyaona kule chini kwa watoa huduma wenzetu ili kubaini nini wanakwama na nini wajibu wetu kama kamati kuweza kuwafikia na kusuruhisha yale ambayo wamekuwa wanakabiliana nayo.” Amesema Kahurananga.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.