Halmashauri ya Wilaya ya Iramba imefanya kikao cha Kamati ya Lishe ili kujadili taarifa ya utekekelezaji wa Afua za Lishe kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2024/2025 ambacho kimefanyika 29/07/2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Kikao hicho kimeongozwa na Mkuu wa Idara ya Idara ya Mipango na Uratibu Ndug. Elikana Zabron kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na kimeketi kujadili taarifa hiyo kwa Kitengo cha Huduma za Lishe, Idara ya Elimu ya awali na Msingi, Idara ya Elimu Sekondari, Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Divisheni ya Maendeleo ya Jamii pamoja na ofisi ya Meneja wa RUWASA Wilaya ya Iramba.
Akizungumza katika kiako hicho Zabron ametoa rai kwa wajumbe wa kikao kwenda kuyatekeleza yote yaliyojadiliwa katika kikao hicho ikiwa ni pamoja na kwenda kutumia fedha kama ilivyo elekezwa katika afua hizo muhimu za lishe.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.