KIKAO CHA KAMATI YA LISHE NGAZI YA HALMASHAURI KWA KIPINDI CHA ROBO YA TATU YA MWEZI JANUARI HADI MACHI 2024 CHAFANYIKA
Halmashauri ya Wilaya ya Iramba imefanya kikao cha Kamati ya Lishe ili kujadili taarifa ya utekekelezaji wa Afua za Lishe kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/2025 ambacho kimefanyika Mei 19, 2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Kikao hicho kimeongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Usafi wa Mazingira na udhibiti Taka Ndug. Jeremia Kahurananga kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri na kimeketi kujadili taarifa hiyo kwa Kitengo cha Huduma za Lishe, Idara ya Elimu ya awali na Msingi, Idara ya Elimu Sekondari, Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Divisheni ya Maendeleo ya Jamii.
Akizungumza katika kiako hicho Kahurananga ametoa rai kwa wajumbe wa kikao kwenda kuyatekeleza yote yaliyojadiliwa katika kikao hicho ikiwa ni pamoja na kuhakikisha afua za Lishe zinatekelezwa ipasavyo kama zilivyokusudiwa.
“Twende tukayatekeleze tuliyo yajadili kwa umakini ili kufikia malengo tuliyokusudia katika kutekeleza afua za Lishe .” Amesema Kahurananga.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe kwa robo ya Tatu Afisa Lishe wa Halmashauri Mary Assey amesema kwa kipindi hicho Jumla ya akina mama/walezi 22,301 (100%) wenye Watoto wenye umri wa miezi 0-23 wamepewa elimu juu ya unyonyeshaji wa watoto wachanga na ulishaji wa Watoto wadogo kupitia watoa huduma ngazi ya vituo vya kutolea huduma za afya, na 7,976 (100%) wamepewa elimu hiyo kupitia watoa huduma ngazi ya jamii.
Pia, jumla ya akina mama wajawazito 13,302 (97.92%) kati ya wajawazito 13,482 waliohudhuriwa kliniki ya uzazi na mtoto, walipewa vidonge vya kuongeza damu, vidonge vya madini chuma na asidi ya foliki vya kutosha hadi hudhurio linalofuata.
Kwa upande wa utoaji chakula shule za Msingi na Sekondari, jumla ya shule 138 (98.6%) kati ya shule 140 zimefanikiwa kutoa chakula kwa wanafunzi angalau mlo mmoja kwa siku. Na jumla ya wanafunzi 69084 (99.8%) kati ya 78480 wanapata chakula muda wawapo shuleni.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.