Mkuuwa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Emmanuel Luhahula amezipongeza kamati mbalimbali zilizoshirikiana kukamilisha zoezi zima la upokeaji wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa, wilayani hapa mwezi Agosti 12, 2018..
Mhe, Luhahula ameyasema hayo leo kwenye kikao cha Tathimini ya Mwenge kilichohusishaU wasilishwaji wa kamati zote za Wilaya zilizoshiriki katika kufanikisha zoezi zima la Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Wilayani Iramba Asilimia Mia moja.
“Sikuzote huwa nawaambia wakuu wangu wa idara na wataalamu, leo mimi ni Mkuu wa Wilaya, lakini tukikaa hapa na kuanza kuonyesha vyeti huenda wengi wananizidi. Kwahiyo siyo kwasababu wewe upo kwenye Kata hautoi ushirikiana kwenye Wilaya. Tunachojaribu hapa ni kushirikiana na kujenga umoja wetu. Umoja wetu ndio ushindi wa Iramba, ndiyo mafanikio yetu.” Alisisitiza Mhe, Luhahula.
Mheshimiwa Luhahula amewataka Viongozi wa Halmashauri na watendaji wa Kata kushirikiana nakuhakikisha wanasimamia vizuri mapato ya fedha wanayoyapata na kuyakusanya kupitia vyanzo mbali mbali vya mapato.
Aidha ameongeza kusema “Kama watendaji wa Kata wakisimama vizuri kabisa, basi Halmashauri haiwezi kupata uhaba wa fedha, na vile vile kama Halmashauri ikiwasimamia vizuri watendaji Kata basi kila kitu kitakwenda sawa.”
Mhe, Luhahula amempongeza aliyekuwa Mratibu wa mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Iramba Ndg, Mashaka Mabuyu kwa mafanikio makubwa aliyoyapata katika kipindi chake cha uongozi wa takribanimiaka 11.
Wanakamati walioshiriki katika kufanikisha zoezi zima la Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2018 wakiwa kwenye picha ya pamoja.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.