KIKAO CHA TATHMINI YA MKATABA WA LISHE JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA NGAZI YA HALMASHAURI KWA ROBO YA PILI KUANZIA MWEZI OKTOBA HADI DISEMBA 2024.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda ameongoza kikao Cha tathmini ya mkataba wa lishe jiongeze na tuwavushe salama kilichofanyika Januari 22,2025 kwenye Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
DC Mwenda amepongeza mafanikio katika usimamizi na utekelezaji wa suala ya lishe wilayani Iramba hasa utoaji wa chakula shuleni ambapo jumla ya shule 140 sawa na asilimia 100 zimefanikiwa kutoa chakula kwa wanafunzi angalau mlo momja kwa siku, na jumla ya wanafunzi 76107 (99.57%) kati ya 77211 wanapata chakula cha mchana muda wawapo shuleni.
Aidha Mwenda ametoa wito kwa Watumishi wa idara ya Afya kuendelea kuwahudumia kwa upendo akina mama Wajawazito na kutoa Elimu ya lishe kwa Jamii inayowazinguka
"kubwa lingine ambalo tumeendelea kuhamasishana na bado halijafanyika kwa kiwango likubwa ni kuhusu kuwa na bustani za mboga mboga kwenye shule zetu, bado shule nyingi kwenye suala la bustani za mboga mboga limekwama. Kwa pamoja tunahitaji kuongeza juhudi ili kuhakikisha kwamba shule zetu hizi zinazalisha mboga kwaajili ya watoto kutumia pale shuleni." Amesema DC Mwenda
Kwa upande wake Afisa Lishe Wilaya ya Iramba Bi. Naomi Sillah amesema kuwa kwa kipindi Cha robo ya pili Mama Wajawazito 11979 (99.6%) kati ya 12027 walihudhiria kliniki ya uzazi na mtoto, kupewa vidonge vya kuongeza damu vya madini chuma na asidi ya Foliki.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.