Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda ameongoza kikao Cha tathmini ya mkataba wa lishe jiongeze na tuwavushe salama kilichofanyika Novemba 11,2024 kwenye Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
DC Mwenda amepongeza mafanikio katika usimamizi na utekelezaji wa suala ya lishe wilayani Iramba hasa utoaji wa chakula shuleni ambapo jumla ya shule 140 sawa na asilimia 100 zimefanikiwa kutoa chakula kwa wanafunzi angalau mlo momja kwa siku, na jumla ya wanafunzi 79400 (99.8%) kati ya 79558 wanapata chakula muda wawapo shuleni.
Aidha Mwenda ametoa wito kwa shule zote ambazo bado hazijafnikiwa katika utoaji wa chakula kwa wanafunzi wote kuhakikisha zinafikia lengo la utoaji chakula kwa wanafunzi wote huku akisisitiza uwepo wa bustani za mboga mboga katika shule zote.
"kubwa lingine ambalo tumeendelea kuhamasishana na bado halijafanyika kwa kiwango likubwa ni kuhusu kuwa na bustani za mboga mboga kwenye shule zetu, bado shule nyingi kwenye suala la bustani za mboga mboga limekwama. Kwa pamoja tunahitaji kuongeza juhudi ili kuhakikisha kwamba shule zetu hizi zinazalisha mboga kwaajili ya watoto kutumia pale shuleni." Amesema Mhe. Mwenda
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.