Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni akiwa na Afisa utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Ndg. B’hango Lyangwa wamekutana na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Kuboresha Utendaji Kazi na Kushughulikia Kero za Watumishi
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni akizungumza na Watumishi katika kikao kazi kilichofanyika leo tarehe 24 julai 2018 katika ukumbi wa Halmashauri aliwaasa watumishi kutoa huduma kwa kuzingatia weledi na kuwajibika katika nafasi zao kwa kutokuwa na ubaguzi kwa Wananchi tunaowahudumia.
Aidha ameongeza kusema kuwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wanatakiwa kuzingatia mkataba wa huduma kwa mteja pale wanapohudumia wateja na kushughulikia kero za wananchi kwa wakati.
Afisa utumishi wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Ndg. B’hango Lyangwa amewaomba watumishi kuwa wavumilivu wakati taarifa zao zinarekebishwa, kwa waliokaribia kustaafu na wale ambao wanastahili kupandishwa vyeo ili walipwe stahili zao kabla ya kustaafu, huku akiwataka wale waliokwisha staafu wakiwa na barua za kupandishwa vyeo kujaza fomu kupitia kwa mwaajiri wao ili waweze kupata stahili zao kwani hakuna haki na stahili ya mtumishi wa umma itakayopotea.
Ndg. B’hango Lyangwa amewataka watumishi wote kujisajili katika tovuti ya watumishi (watumishi portal) ili wawe na uwezo wa kuona taarifa zao za kiutumishi na kuweza kufuatilia masuala yao ya kiutumishi yamefikia katika hatua gani.
Ndg. B’hango Lyangwa amewahakikishia watumishi kuwa taarifa zote za kwenye mfumo zinakua ni taarifa safi na zilizo kamilika kwa kuhakikisha kwamba watumishi wana tarehe kamili na sahihi za kuzaliwa, tarehe zao za ajira, tarehe zao za kila mara walipopandishwa vyeo, taarifa zao za mifuko kwenye hifadhi ya jamii, sifa zao za kielimu, vyeo walivyonavyo pamoja na masuala mengine.
Baadhi ya watumishi kutoka katikaHalmashauri ya Wilaya ya Iramba wakifuatilia kwa makini yaliyokua yakiendelea wakati wa Kikao katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba leo.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.