Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025 Ndugu lsmail Ussi ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Makaravati 10, Daraja la mita 50 na Barabara yenye urefu wa Km. 1.5 uliopo kijiji cha Konkilangi wilayani Iramba mradi unaogharimu thamani ya Tsh Bilioni 6.7.
Awali akizungumza na wananchi katika kijiji hicho Julai 21, 2025 Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe. Suleiman Mwenda amesema kuwa mradi huo wa ujenzi wa daraja hilo utakua na awamu mbili za utekelezaji kutokana na ukubwa wa daraja hilo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa hatua ya pili ya utekelezaji wa mradi huo itaimarisha barabara hiyo kuanzia eneo la mlandala hadi kufikia eneo la Simiti. Pia amewataka wananchi kuitunza miundombinu hiyo pamoja na kuzingatia usalama wao mara baada ya miundombinu hiyo kukamilika.
Mradi huu utakapokamilika utasaidia Barabara hiyo kupitika muda wote, tofauti na ilivyo kuwa awali.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.