KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA 2025 AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA UJENZI WA KIWANDA CHA KUKOBOA MPUNGA TYEGELO UNAO MILIKUWA NA KUKIKUNDI CHA VIJANA CHA NGUVU MOJA IRAMBA
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ndugu lsmail Ali Ussi, Julai 21, 2025 ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kukoboa Mpunga Tyegelo unao milikuwa na kukikundi cha vijana wajasiriamali Nguvu Moja Iramba.
Mradi huo una thamani ya shilingi milioni 22, ikiwa ni sehemu ya mkopo wa asilimia 10 unaotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Utoaji mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ni utekelezaji wa agizo la serikali la kuhakikisha mikopo ya asilimia 10 inawanufaisha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, hatua inayolenga kuwawezesha wananchi kiuchumi.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.