KITUO CHA AFYA TYEGELO CHAZINDULIWA RASMI TAYARI KWA AJILI YA KUANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA NA KUPUNGUZA CHANGAMOTO ZA AFYA KWA WANANCHI KAMA SIYO KUZIONDOA KABISA
Wananchi wa Kata ya Kidaru,Tarafa ya Kisiriri Wilaya ya Iramba Mkoani Singida,Wametakiwa kumwonyesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani,Uungwana wa kumpigia kura za Ndiyo kwa kazi kubwa anazozifanya za kuleta miradi mingi ya Maendeleo kama vile Kituo Cha Afya Tyegelo kilichopo Kata ya Kidaru ambacho ilikuwa ni ndoto kwa Wananchi wa Kata hiyo.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Suleiman Yusuph Mwenda ambaye alikuwa mgeni Rasmi Katika Uzinduzi wa Kituo Cha Afya Tyegelo kilichopo Kata ya Kidaru,Tarafa ya Kisiriri Wilayani Iramba uzinduzi uliofanyika Septemba 16,Mwaka huu katika Kijiji Cha Tyegelo, Tayari kwa kuwahudumia Wananchi wa eneo Hilo la bonde la ufa .
Aidha DC Mwenda amesema takribani Miaka miwili na nusu ya Uongozi wa Rais Samia ametoa miradi mingi sana katika Wilaya ya Iramba pamoja na nchi nzima,Lakini katika Kata ya Kidaru Mama Samia ameleta Miradi katika Shule ya Msingi Mwamapuli,ambapo takribani Milioni 250 zimepelekwa kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba 4 na Madarasa Mawili mapya kwa ajili ya wanafunzi pamoja na Matundu 24 ya Vyoo vya wanafunzi katika Shule hiyo.
Amesema katika Shule ya Sekondari Kidaru serikali imeleta Jumla ya Shilingi Milioni 100 kwa ajili ya Ujenzi wa Madarasa Sita,ikiwemo ujenzi wa Hosteli kwa ajili ya watoto wa kike ambao uligharimu Shilingi Milioni 70 kwa ajili ya ukamilishwaji wa jengo hilo.Hata hivyo ameongeza kuwa siyo hivyo tu na Shule ya Msingi Kidaru nako serikali ikatoa Shilingi Milioni 11 kwa ajili ya umaliziaji wa Darasa moja,Ujenzi wake Tayari umekamilika.
Kiongozi huyo akiwaleleza Wananchi kazi zilizofanywa na serikali ya awamu ya Sita,inayoongozwa na Mama Samia,amesema si hivyo tu hata barabara ambayo inatoka Kidaru Tyegelo Luono hadi Makao makuu ya Wilaya Kiomboi lakini Fedha zililetwa na serikali ambazo ni Bilioni 3 na Milioni 500 ambazo sasa zinajenga karavati katika barabara ya Tyegelo hadi Ndurumo na kuelekea Mto Sibiti na inatarajiwa kijengwa kwa Kiwango cha lami
DC Mwenda ameeleza kuwa hivi "Hapa tulipo Leo tunazindua Kituo Cha Afya Tyegelo Kata hii ya Kidaru ,Kituo ambacho ilikuwa ni ndoto lakini mama kwa huruma zake kwa Wananchi wa Kata ya Kidaru akatoa Tsh. Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo hiki ambapo Leo Tunakizindua" amesema DC Mwenda.
Licha ya hayo amesema pia Jumla ya Tsh. Milioni 800,Zimenunua vifaa tiba kwa lengo la kutoa huduma Bora na za kisasa .
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.