Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Mhe, Emmanuel Luhahula ameongoza Kogamano la kupolomoka kwa maadili ya watoto/vijana wa taifa letu limefanyika leo katika ukumbi mkubwa wa halmashuri Wilayani iramba mkoa wa singida liloandaliwa na jumuiya ya wazazi Wilaya na Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Iramba. Kauli Mbiu Wazazi tupo imara kutekeleza maadili ya Taifa letu.
Mhe. Emmanuel Luhahula ameungana na Mwenyekiti wa Halmashuri ya Wilaya ya Iramba Mhe. Simion Tiyosera, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mwl Linno Mwageni, viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba na wananchi kuadhimisha kongamano la kupolomoka kwa maadili wa watoto/vijana wa taifa letu.
Mhe. Luhahula amewataka wazazi kuwajali na kuwapenda watoto wao kwa kuwalea, kuwapatia maadili mazuri na kuwakinga na ukatili wa kijinsia. Ameongeza kwa kusema wazazi wanawajibika kikamilifu katika kuhakiksiha watoto wao wanapata elimu, kuwalinda na ukatili wa kijinsia pamoja na kupinga ndoa za utotoni ambazo zinawakatisha watoto masomo.
Pia ameongeza kwa kusema wazazi wasiache watoto wao kufanya wanachotaka, kama amefanya kosa anastahili ahadhibiwe ili afundishwe kilicho chema. “Watoto wanastahili wapewe misngi mizuri ya maadili na wazazi, walezi na Viongozi mabilmbali tuwalee watoto wetu kwenye misngi ya madili. Alisema Luhahula
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Mhe. Emmanuel Luhahula ameagiza wote walihusika na ubadhirifu wa fedha kwenye chama cha ushirika cha MWAI kiasi cha Zaidi ya Shilingi milioni 180 wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia mara moja.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.