"Mimi mkuu wenu wa Wilaya kutokana na changamoto mbalimbali tunazozipokea, tunaposikiliza na kutatua kero za wananchi na wakati mwingine zinakuja moja kwa moja ofisini kwangu tukaona upo umuhimu wa kuweka kambi ya siku nne ya Madaktari bingwa ambao watatoa huduma za kibingwa hapa hapa Wilayani kwetu " Mwenda amesema.
"Kwa hali hiyo kwa kweli tunazo Rufaa nyingi sana kwa watu wetu wanaotoka katika vituo vyetu hapa Wilayani na wanaotaka kwenda Hospitali kubwa zenye Madaktari bingwa, Kwa Mwaka Jana, Zaidi ya watu 138 walifika Hospitali kwa kupewa Rufaa, Hivyo ukipiga mahesabu kwa mwezi karibu watu 14 wanapewa Rufaa na wengine 59 hadi 60 wanaohitaji matibabu ya Kibingwa hivyo tumeona tuwapunguzie Mzigo kwa kuwaletea hawa Madaktari bingwa ili watu hawa watibiwe wakiwa Wilayani kwao" Ameongeza , DC Mwenda.
Mkuu wa Wilaya ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kampeni ya matibabu ya Madaktari bingwa pia amesema " Ni mshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuboresha na kuimarisha Sekta ya Afya kote Nchini, Sisi katika Hospitali yetu ya Wilaya ametupatia Vifaa kwa Mwaka Jana , Vifaa 129 ambavyo hata vingine bado havina wataalamu wa kuvitumia vyenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni moja Milioni Mia nne themanini na moja".
Akitoa taarifa kwa Mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu Wilaya Daniel Paul amesema wao katika Hospitali ya Wilaya Wanamuunga mkono Rais Samia kwa kazi kubwa ya kuboresha Miundombinu ya Afya kwani Mwaka wa fedha 2023/2024 walipokea vifaa vyenye thamani ya Bilioni moja na Milioni Mia nne themanini na moja, na siyo hivyo tu "Mheshimiwa bali tunao mtambo Mkubwa wa Kuzalisha hewa ya oksijeni ambao uko mbioni kuanza kufanya kazi" Amesema Daniel.
Naye Daktari Bingwa George Kanani ambaye ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Jumla kutoka Bugando amesema lengo Lao ni kusogeza huduma za kibingwa, Kiomboi ili kusaidia wananchi wenye mahitaji ya Kibingwa ili wananchi waweze kupata huduma bora, amesema huduma hiyo ni endelevu hivyo wananchi wasipate mashaka kwa hilo.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.