Hemedi Munga, Irambadc
tehama@irambadc.go.tz
Iramba. Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amemuagiza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Simion Tiyosera kuchukua hatua zidi ya watumishi wafujaji wa mapato ya Halmashauri ambao wanaikwamisha Halmashauri.
Luhahula ameyasema hayo katika kikao kazi leo Agosti 21, 2019 katika ukumbi wa Halmashauri wilayani Iramba na kuwataka takukuru kuchunguza kwa kina pamoja na kuwachukulia hatua wale wote wanaofuja na kukwamisha mapato ya Halmashauri.
Hatua hiyo inawajengea watumishi ari ya kazi inayoongeza mapato ya Halmashauri na kuifanya Halmashauri kutimiza malengo yake. Ameongeza Luhahula
Akiongea katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri, Simion Tiyosera amesema wanatumia sheria mama kuanzisha chanzo cha mapato kwa kuchukua asilimia tano kukusanya mapato yanayosimamiwa na wasimamizi wa mapato ambapo umeifanya Halmsahauri ya Iramba kutembea katika reli kati ya halmsahuri saba mkoani Singida.
Tiyosela amewasifu wakusanyaji wa mapato wanaoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Linno Mwageni na Mweka Hazina na timu yake kwa kuweka mianya ya kuzuia rushwa kwenye ukusanyaji wa mapato kwa kuweka kwenye kila kijiji mtendaji mwenye POS anayekusanya mapato na pesa hiyo inapofika Halmashauri mtendaji anarudishiwa asilimia 20%.
Akiongea katika kikao hicho mkuu wa takukuru wilayani Iramba, Deo Mtui amewataka watumishi wa Halmashauri ya Iramba kuzaliwa upya kudhibiti na kuziba mianya ya rushwa.
Hatua hiyo utaifanya Halmashauri kukusanya mapato yake yatakayosababisha kuunga mkono juhudi za Mh, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kuipeleka nchi katika uchumi wakati. Aliongeza Mtui
Mtui ameitaja mianya ya rushwa ambayo kwa mujibu wa sheria ya kupambana na kuzuia rushwa inachangia uwepo wa rushwa kwa wadau wanaotoa huduma na wale wanaopokea huduma. Huku akiwataka watumishi kujiepusha na mianya hiyo.
Amebainaisha mianya hiyo inayotokana na sheria mbovu za ukusanywaji wa mapato katika wilaya ya Iramba, mwanya wa rushwa unaotokana na ufanisi mbovu wa mifumo ya kieletroniki katika ukusanyaji wa mapato wilayani Iramba, mwanya wa rushwa unaotokana na sababu za kutofikia kwa malengo ya ukusanyaji wa mapato.
Huku akimalizia kutaja mwanya wa rushwa unaotokana na mmomonyoko wa maadili kwa baadhi ya watumishi wanaosimamia ukusanyaji wa mapato na kukosekana mikakati ya kuzuia rushwa katika Halmashauri ya wilaya ya Iramba.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.