By Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni amepokea tuzo ya Kitaifa ya Shule ya Sekondari Lulumba.
Mwageni amepokea tuzo hiyo leo Jumatano Oktoba 30, 2019 wakati akiongea na Mkuu wa shule na baadhi ya walimu wa Lulumba Sekondari.
Tuzo hiyo ilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo, kwa kuwa Lulumba Sekondari ni miongoni mwa shule zinazoendelea kwa muda wa miaka mitatu mfululizo.
Akiongea na mwandishi wetu, Afisa Elimu Sokandari, Godfrey Mwanjala amesema shule ya Lulumba Sekondari ni miongoni mwa shule zinazoendelea kwa muda wa miaka 3 mfululizo na kufanikiwa kushika nafasi ya 5 kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita 2019.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, amemuagiza Afisa Taaluma Sekondari, Patricia Ngaa kuhahikisha wanapokuwa wanafanya tathimini ya matokeo yaendane na maonesho ya shughuli za ubunifu zinazofanyika katika shule zetu.
Huku akimtaka kuhakikisha kunakuwa na uwakilishi wa kila shule.
“Tutaongeza nafasi za vijana wetu tunaowafundisha kuwa wabunifu” Amesema Mwageni
Mwageni amewapongeza walimu kwa kutumia taaluma zao walizozisomea na kile ambacho kinachofanyika.
“Mmefanya makubwa na yamejionesha kwa dhati” Aliongeza Mwageni
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Lulumba Sekondari, Jeremia Mungwe amempongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa ushirikiano anoutoa kwa shule hiyo.
Mungwe amemkabidhi Mkurugenzi Mtendaji tuzo ya kitaifa iliyoipata shule hiyo kutokana na ufaulu mzuri wa kidato cha sita 2019, huku akimuhakikishia kuwa walimu wanahamasa na kumuahidi kuwa ufaulu huo utakuwa endelevu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni akiwa na baadhi ya walimu wa Lulumba Sekondari wakishangilia tuzo ya kitaifa iliyoipata Lulumba Sekondari kufuatia kupata ufaulu mzuri katika matokeo ya kidato cha sita 2019.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.