Mkuu wa Wilaya ya iramba mkoani Singida Suleman Yusuph Mwenda Amezitaka Sekta za serikali zilizoko kuunga mkono juhudi Zinazo fanywa na Wanawake katika kujikomboa Ki-Uchumi na kuhakikisha kuwa na Usawa wa kutoa fursa sawa Kwa Wanawake na wanaume.
Aidha kuhusu ugonjwa wa Ukimwi kiongozi huyo amewataka Wananchi kujitokeza kupima Kwa hiari Kwa Lengo la kujiepusha na maambukizi Kwani Mwaka Jana 2022 Watu mia Tisa Waligundulika kuambukizwa vvu baada ya Watu Elfu 65056 kujitokeza kupima vvu na Ukimwi Kwa hiari.
Hayo yote yamejiri katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika Kata ya Kidaru Tarafa ya Kisiriri Wilayani Iramba mkona Singida.
Hata hivyo kiongozi huyo Amewapongeza Wananchi wa Kijiji na Kata ya Kidaru Katika kujitolea kwao kuchangia fedha na nguvu zao katika Miradi ya maendeleo bila kujali kuwa serikali inatoka fedha Kwa ajili ya Miradi hiyo.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.