
Maandamano ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika viwanja vya chuo cha Ualimu Kinampanda Wilayani Iramba
Katibu tawala wa wilaya ya Iramba mkoani Singida ambaye ni mgeni rasmi katika siku ya wanawake duniani Ndg: Pius S. Songoma akiwa na Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Ndg: Emmanuel Makwaya na Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Iramba wameadhimisha siku ya wanawake iliyofanyika viwanja vya chuo cha Ualimu Kinampanda Kata ya Kinampanda Wilayani Iramba mkoani Singida.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa tarehe 8 Mwezi wa 3 kila Mwaka. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “BADILI FIKRA KUFIKIA USAWA WA JINSIA KWA MAENDELEO ENDELEVU”. Dhamira ya kauli mbiu ya siku ya wanawake Duniani ni kuhamasisha jamii nzima pamoja na wadau nchini kutoa fursa mbalimbali kwa upande wa wanawake ili kuweza kunufaika na fursa za kimaendeleo.
KIOMBOI, IRAMBA
Postal Address: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Telephone: 026 - 2532253
Mobile: 026 - 2533001
Email: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.