Mkuu wa Wilaya ya Iramba ambaye alikuwa Mgeni rasmi kwenye siku ya Wanawake Duniani Wilayani Iramba Mkoa wa Singida Mhe: Emmanuel Luhahula akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni na Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Iramba wameadhimisha siku ya wanawake Duniani iliyofanyika Kata ya Shelui Wilayani Iramba.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa tarehe 8 Mwezi wa 3 kila Mwaka. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA TUIMARISHE USAWA WA JINSIA NA UWEZESHAJI WANAWAKE VIJIJINI”. Dhamira ya kauli mbiu ya siku ya wanawake Duniani ni kuhamasisha jamii nzima pamoja na wadau nchini kutoa fursa za Kiuchumi kwa upande wa wanawake ili kuweza kunufaika na fursa za kimaendeleo kuelekea katika kipindi cha Tanzania ya uchumi wa viwanda.
Katika Sikukuu hiyo, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba imetenga fedha za Mikopo Shilingi Milioni 61 kwa vikundi Ishirini na Tisa ili kuviwezesha kuimarisha Biashara yao pia kuimarisha Wanawake vijijini pia Mkuu wa Wilaya ya Iramba amewaasa wanavikundi wote waliopatiwa Mikopo kutumia Mikopo hiyo vizuri.
Maandamano ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kata ya Shelui Wilayani Iramba Mkoani Singida.
Kikundi cha Wanawake kinachomiliki kiwanda cha kukamua Mafuta ya Alizeti
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.