• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Comments |
Iramba District Council
Iramba District Council

The United Republic of Tanzania Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Iramba District Council

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Sura
    • Maadili ya Misingi
    • Mikakati
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
    • Afya
    • Kilimo
    • Elimu
    • Maji
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Utawala
    • Idara
      • Mipango, Takwimu & Ufuatiliaji
      • Afya
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Idara ya Ardhi na Mipango miji
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Fedha na Biashara
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mazingira na Usafishaji
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA NA UHUSIANO
      • Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo Cha Ufugaji Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF
    • Muundo wa Halmashauri
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Riport
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
      • Fomu za Maombi kwa Wateja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao Mbalimbali
  • Salary Slip

MAAFISA ELIMU KATA 136 MKOANI SINGIDA WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU USIMAMIZI WA SHULE NA UJAZAJI TAKWIMU KATIKA MFUMO WA "SIS"

Posted on: March 24th, 2025

MAAFISA ELIMU KATA 136 MKOANI SINGIDA WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU USIMAMIZI WA SHULE NA UJAZAJI TAKWIMU KATIKA MFUMO WA "SIS"


Maafisa elimu Kata 136 mkoani Singida wamepatiwa mafunzo maalumu kuhusu Usimamizi Saidizi katika maeneo yao ya uongozi wa shule na ujazaji wa takwimu katika Mfumo wa "School Information System" (SIS). Mafunzo hayo yamefanyika 24/03/2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, yakihudhuriwa na viongozi wa elimu ngazi ya Mkoa, Wathibiti Ubora wa shule Mkoa na Wilaya, Wakuu wa Divisheni Elimu ya Awali na Msingi, yakiongozwa na wawezeshaji kutoka ADEM na TAMISEMI.


Akifungua mafunzo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Elipidius Baganda amepongeza juhudi za maafisa elimu Kata katika kutekeleza majukumu yao, akibainisha kuimarika kwa ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya taifa. Aidha, ameutambua mchango wa Mradi wa Shule Bora katika kuboresha ufundishaji wa walimu na ujifunzaji kwa wanafunzi wote wakiwemo wenye mahitaji maalumu kutokana na weledi wa walimu kupitia mafunzo mbalimbali yanayofanyika katika halmashauri zote za mkoa wa Singida. Na amewasihi wadau wa elimu kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha elimu kwa ngazi zote, ikiwemo elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi.


"Mafunzo haya yanalenga kuwaongezea ujuzi maafisaelimu Kata ili waweze kusimamia ipasavyo shughuli za elimu katika maeneo yao, hususani katika kuhakikisha ujazaji sahihi wa taarifa za shule kwenye Mfumo wa SIS." alisema Dkt. Baganda


Pia, Amesisitiza umuhimu wa kuongeza ufaulu wa wanafunzi, kukamilisha miundombinu kwa ubora, kutoa taarifa za maendeleo kila wiki, huku akiwakumbusha watumishi wa umma kutojihusisha na siasa.


"Hakikisheni ufaulu wa wanafunzi unaongezeka, miundombinu ya shule inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa, taarifa za maendeleo zinatolewa kila mwisho wa wiki. Pia, ni muhimu mtumishi wa umma kuepuka kujihusisha na masuala ya kisiasa, ili kuepusha mgongano wa maslahi." alisema Dkt. Baganda


Shule Bora ni mradi wa Serikali unoatekelezwa kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na TAMISEMI, ukisimamiwa na Cambridge Education kama mshauri na kufadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia FCDO. Mafunzo hayo yametolewa na wawezeshaji Guido Kinomko na Ester Jonas kukoka ADEM Pamoja na Nestory Ngimwa kutoka TAMISEMI.





Announcements

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU January 02, 2026
  • ZOEZI LA CHANJO YA KITAIFA YA HOMA YA MAPAFU KWA NG'OMBE, SOTOKA KWA MBUZI NA KONDOO, NA MDONDO KWA KUKU January 08, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KWA ROBO YA PILI YA MWAKA WA FEDHA 2024/2025. March 12, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI June 05, 2025
  • View All

Latest News

  • MAONESHO YA MATUMIZI YA PEMBEJEO ZA KILIMO (MBEGU, MBOLEA NA VIUATILIFU) HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA DISEMBA 29-30, 2025

    December 28, 2025
  • HERI YA SIKUKUU YA KRISMASI NA MWAKA MPYA 2026

    December 25, 2025
  • DC MWENDA AWATAKA WALIMU IRAMBA KUONGEZA UBUNIFU NA BIDII KUINUA UFAULU

    December 09, 2025
  • HERI YA MIAKA 64 YA UHURU WA TANZANIA BARA

    December 09, 2025
  • View All

Video

wanafunzi wakiimba wimbo wa TAZAMA RAMANI katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika wilayani Iramba
More Videos

Quick Links

  • Organisation Structure
  • Mission and Vision
  • Reports
  • Water Department

Related Links

  • OFISI YA RAIS-TAMISEMI
  • OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA
  • WATUMISHI PORTAL
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
  • SEKRETARIETI YA AJIRA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    KIOMBOI, IRAMBA

    Postal Address: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA

    Telephone: 026 - 2532253

    Mobile: 026 - 2533001

    Email: ded.irambadc@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.