MAAFISA VIUNGO WA BAJETI IRAMBA WAPEWA MAFUNZO YA UANDAAJI WA MIPANGO NA BAJETI
Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kupitia Idara ya Mipango na Uratibu, imeendesha mafunzo ya Mipango na bajeti kwa maafisa Viungo wa Bajeti wa Idara na Vitengo ili kuwa na uelewa wa pamoja juu ya masuala ya upangaji na utekelezaji wa Bajeti kuelekea maandalizi ya bajeti ya mwaka wa Fedha 2026/2027.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Octoba 1, 2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Ndg. Michael Matomora amewataka Maafisa Bajeti hao kuzingatia muongozo wa uandaaji wa bajeti baada ya kupewa mafunzo ambayo yatawawezesha kurahisisha zoezi la uaandaji wa bajeti, ili waweze kuandaa bajeti kwa kuzingatia vipaumbele vya Wananchi na Halmashauri.
"Pangeni bajeti kwa kuanza kuainisha mahitaji na vipaumbele, na kuona kipi kianze kutekelezwa sasa na kipi kifuate baadae. Baada ya kujua mahitaji yote na vipaumbele, ainisheni vyanzo vya mapato na kiasi kinachoweza kukusanywa." Amesema DED Matomora.
Mafunzo hayo yana lengo la kuwawezesha Maafisa Viungo wa Bajeti kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao. Pia, yatawawezesha Maafisa hao kuhakikisha maandalizi, usimamizi na ufuatiliaji wa Mipango na Bajeti unafanyika kwa kuzingatia taratibu na miongozo.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.